UKAWA INATAKA KUSHINDA AU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU 2015?
UKAWA inataka kushinda Uchaguzi au inataka Kushiriki Uchaguzi?
Yericko Nyerere
Kushindwa kwa upinzani nchni kwa kiwango kikubwa katika chaguzi hizi kunatokana na muundo wa vyombo vya maamuzi ya uchaguzi wa nchi yetu, mathalani, Katiba, Tume.
Kwasasa Katiba inasema kuwa matokeo ya urais hayatahojiwa na mtu yeyote ama chombo chochote wala mahali popote, hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa Tume anayechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM na anayelipwa na Mwenyekiti wa ccm akitangaza jina fulani hata kwa bahati mbaya tu baai haruhusiwi kurekebisha.
Mwaka 2010 baada ya kushindwa uchaguzi mkuu, Upinzani chini ya Chadema uliituhumu sana tume Uchaguzi kwakuchakachua matokeo ambayo ilipoka ushindi wa 64% wa Dr Slaa malalamiko yao ndiyo yalipelekea kuwepo mchakato wa kuandika katiba mpya.
Mchakato huo umeishia kwa zengwe la CCM kuvuruga maoni ya umma na kuweka maoni yao ambayo ni kinyume kabisa na matakwa ya umma,
Maridhiano ya upinzani na msanii wa ccm baada ya dalili za uwepo finyu wa katiba Mpya yalikuwa ni kuiboresha katiba ya 1977 hasa zile ibara za kidikteta mfano, uundwaji wa Tume Huru, Matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani, nk ili utuongoze kwenye Uchaguzi wa 25/10/2015.
Haya ndiyo mambo mtambuka zaidi dhidi ya mstakabali wa taifa letu, na ilitarajiwa marekebisho hayo yawasilishwe kwa hati ya dharula kama ilivyowasilishwa miswada ya kupiga marufuku watu kuisema vibaya ccm na serikali yake,
Sasa nashangaa Upinzani unataka kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwingine chini ya tume ile ile, Katiba ileile, uwanja uleule. Hakuna kilichobadilika kati mwenendo na mazingira ya uchaguzi wa 2010 na huu tunaotarajia kuufanya kesho.

Kitakachosaidia ushindi wa UKAWA na Kwenda Ikulu sio Tume hii ya Boss wa Ccm, bali nguvu ya umma. Watanzania wakapige kura ili kujipa uhalala wa kuingia vitani rasmi,
Vita ya Ukombozi ina mkono wa Mungu!
Ili kuondokana na misuguano mikali ya ccm kukabidhi ofisi hapo 25/10/2015, kwa vyovyote vile kunahitajika masuala mawili mhimu ya dharura.
1. Tume huru ya Uchaguzi.
2. Uwezekano wa matokeo ya uraisi kuhojiwa mahakamani.
Hayo ni mambo mhimu sana kwa sasa, lakini kwasasa si mhimu tena kwakuwa yamefifishwa na muda, kilichobora kwa sasa ni maandalizi ya vita ya kiutu yenye tone la damu kutua ardhini kwa heshima dhidi ya udharimu huu wa ccm.

Comments
Post a Comment