BENSON KIGAILA AONESHA UWEZO WA KIPEKEE KATIKA KUPAMBANUA MAMBO



Na Mhere Mwita
Majira ya saa 2:30 Ndugu Benson Kigaila ambaye ni mkurugenzi wa organization ya CHADEMA ngazi ya Taifa na ni mtia nia ubunge jimbo la Dodoma mjini alifanikiwa kufanya mdahalo na wanachama ,baadhi ya viongozi na watia nia wa  Ubunge na Udiwani toka sehemu mbalimbali za nchi.Kijana haya alijidhihirisha kuwa anauwezo wa kipekee na ana kaliba ya kiuongozi kwa kujib maswali kwa ufasaha zaidi ya matarajio ya wengi.

Uwezo wake ulitambulisha kuwa CHADEMA ina hazina kubwa ya viongozi tens waliomakini nitaweka baadhi ya maswali na majibu aliyoulizwa na wajumbe hao hapa chini:-

swali 1:Kwanini umeamua kugombea ubunge?
Majibu:Nimeamua kugombea ubunge kwa lengo la kusaidia kujenga jamii ya watu walio sawa mbele ya sharia,jamii guru na inayongozwa kwa haki na kuwatatulia kero zinazowakabili sasa ambazo waliopita hawajazitatua hadi leo kwa mfano Tatizo la Ardhi ya watu wa Dodoma dhidi ya CDA,ni tatizo kubwa linalohitaji mtu anayelijua na ana dhamira ya dhati kulitatua aliweka ufafanuzi tatizo la maji ,Elimu na Afya lakini alisisitiza kutekeleza ilani na Sera za chama

Swali 2:-Ni Changamoto gani ambazo unakutana Nazi kama kiongozi wa taasisi kubwa CHADEMA?
Majibu:Changamoto kubwa kuliko zote ni namna ya kuwafikia wananchi wengi wanaotaka kufikiwa kwa wakati mmoja.

Aliulizwa maswali mengi ya kumjenga na kuwajenga watia nia wengine ,Aidha alipoulizwa ni nani role model wake katika siasa?Alimtaja Mwl.J.K Nyerere ,Patric Lumumba na viongozi wake wa CHADEMA
Pia aliweza kuwashauri viongozi wote wa chama kufuata taratibu na kanuni za chama kwa mjibu wa katiba ili kuvunja makundi yanayoendelea baina ya watia nia na akawaasa watia nia wote kujenga umoja na kufanya kazi kwa pamoja kwani lengo sio kuonekana mtu ni diwani au mbunge bali ni kuifanya jamii mpya.
Alisisitiza mshikamano kwa kipindi hiki cha mapambano.
Bensoni ameonekana kuwa ni zaidi ya kiongozi pale aliposema kuwa yupo tayari kufanya kazi na kuwasaidia watakaoshinda kwenye kura za maoni hata kama yeye hatapitishwa na chama chake.

Ni mengi yaliulizwa na mengi yalijibuwa lakini kutokana na mda naomba nisikuchoshe usinichoshe niishie hapa tujifunze kukubali matokeo kama alivyotuasa Watia nia wengine.
VIVA CHADEMA

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI