UTAMTENGANISHA VIPI MAKONGORO NA WANACHAMA PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE NDANI YA CCM?

Unamtenganisha vipi Makongoro na wanachama pamoja na viongozi wengine ndani ya CCM?

 Na Yericko Nyerere
Ni baada ya Msafara wa Makongoro kuelekea Kigoma kupata ajali



Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamka kwamba, Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi, rais atachaguliwa kutoka kwenye chama cha siasa, hii inamaana kuwa ni lazima awe mwanachama wa chama cha siasa.

 Katiba ya chama cha mapinduzi inasema kuwa ili uwe mwanachama, ni lazima ukubaliane na Itikadi,falsafa na miiko ya chama cha mapinduzi. Sasa ili chama kiongoze serikali hutumia sera, sera ndio dira ya kuongozea serikali ya chama.

 Ili chama kunadi sera zake huwa kinatanguliwa na Ilani, ilani ya chama ndio dira ya kunadia sera za chama husika mbele ya makutano. Hilo ndilo lilipo kwa vyama vyote vya kidemokrasia duniani.

 Ndani ya ccm mwaka huu wa uchaguzi Ilani na sera yake inaandaliwa na makada mashuhuri wa chama hicho wakiongozwa na Andrew Chenge, Steven Wasira, Asha Rose Migiro, na wajumbe wengine kutoka Zanzibar ambapo mwezi wa nane ilani hiyo itazinduliwa, Hii inamana kuwa ilani hiyo na sera zake ndio itakuwa dira na muongozo wa Makongoro kuongoza nchi kama makada wa chama hicho wanavyojidi.

 Watanzania kwa sasa wameondokewa na imani kabisa na CCM, uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 Wengi waliaminishwa kwamba safari hiyo, baada ya Mzee Rukhsa, CCM inatuletea mgombea stahiki, mtu msafi asiye na tone la kashfa, William Benjamin Mkapa, mzee wa utandawazi au mr. Clean!
 Kwa miaka kumi ya utandawazi wake tuliushuhudia na kuuvumilia huo usafi wake ikiwa ni pamoja na kufanya biashara akiwa Ikulu chini ya Kiwila.

 Mwaka 2005, CCM ilituletea waliyedai ni kijana anayejua matatizo ya Watanzania na hivyo kupewa ridhaa ya uongozi wa taifa hili kwa asilimia 80%! Huyo kijana aliyeingia kimachachari kwa ari na nguvu mpya katumia zaidi ya robo ya muda wake kutalii kwa kisingizio cha kuomba misaada hadi kuchokwa ndani na nje ya nchi yetu.

 Kwa ufanisi mkubwa ameweza kuligawa taifa hili kikanda, kikabila na kidini na hata pale alipooneshwa kushindwa, CCM ilihakikisha anapata awamu ya pili.

 Sasa makada walewale leo wanapendekeza aingie Makongoro Nyerere kwa laghai zile zile kwamba ataleta kipya na kufanikisha mabadiliko, wamesahau kuwa chama ndicho huongoza serikali sio mtu.

 Ingelikuwa nchi za dunia ya tatu wenzetu sera huwa kwenye katiba, vyama haviingii madarakani na sera zao bali vinaingia na mikakati ya utekelezaji wa sera za kitaifa ambo zimeainishwa kwenye katiba.

 Nakuuliza Mtanzania mwenzangu, unamtenganisha vipi Makongoro Nyerere na wanachama wenziye anaoshindana nao, kula nao na kuafikiana nao?

 Zingatia, Makongoro ataendesha nchi kwakufuata sera za ccm, sio sera zake, hivyo sera za ccm kama ni wizi, uuzaji wa madawa ya kulevya, ufisadi na ujangiri, basi Makongoro atakuwa kiongozi mkuu wa makundi hayo ndani ya nchi

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI