HATIMAYE JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI LAPATA MKOMBOZI WAO ATAKAYEWATETEA.
Dr Elias akiwa katika mkutano na wananchi wa kata ya Isange.
Pichani ni Dr Elias akiwahutubia wananchi wa kata ya Isange.
Dr Elias akiwa na wananchi wa kata ya Lutabe jimboni kwake Rungwe mashariki, nyumba kwa nyumba, shamba kwa shamba operation aliyoifanya kwa mienzi zaidi ya miwili hadi sasa anaendelea na operation hii ili kuwakombowa wakazi wa RUNGWE
Hakika penye nia pana njia,jimbo la Rungwe mashariki liliongozwa kwa mda mrefu na mh Prof. Mark Mwandosya lakini hakuweza kuwasemea wananchi matatizo yao bungeni kwa mda mrefu, sijui kwakuwa alikuwa ni Waziri japo sio sababu ya kushindwa kuwasemea wananchi wa jimbo lake.
Inasemekana Mh Mwandosya kashindwa kabisa kuwatetea wakulima wa chai huku akijua kabisa chai ni zao muhimu la biashara kwa wakazi wa Rungwe, lakini hadi sasa wanauza kwa bei ya hasara sana kwa kilo.
Lakini pia kama mbunge hajafanya jitihada za kufufua na kuboresha kiwanda cha chai kilichoko Mwakaleli, hivyo kuwanyima fursa za ajira wakazi wa Busokelo na maeneo mengine ya jirani vilevile ameshindwa kupigania ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Katumba, Mwakaleli, Lwangwa, Mbambo mpaka Tukuyu iliyoahidiwa na Mhe. Kikwete katika kampeni za uchaguzi mwaka 2010.
Si Mwandosya wala si madiwani waliofika kuwapa pole na kuwatetea wananchi wa Lwangwa jimboni kwake baada ya kuvamiwa, kuporwa na kupigwa na polisi usiku. Inasemekana ni viongozi wa CHADEMA pekee waliofika kuwapigania wananchi hao na kupata haki ya kisheria. Ushahidi wa jambo hili ni wananchi wa Lwangwa kuichagua CHADEMA kuiongoza halmashauri ya kijiji yalipo makao ya halmashauri ya jimbo hil kama adhabu kwa CCM
Sasa kilio cha watu wa Rungwe "wakukaja" kimesikika, kijana mwadilifu asiye na makuu, mweledi na ambaye hujali maisha ya watu wake anaowaongoza ameamua kujitosa kuwatetea watu wa Rungwe naye si mwingine ni "Dr. ELIAS KASONSO MWAKAPIMBA" ambaye ni miongoni mwa vijana machachari na mmoja wa watia nia ubunge jimbo la Rungwe Mashariki (Busokelo) kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Nimefanikiwa kupata wasifu wake kiundani na mapito aliyopitia,
Hebu twende sawa tuone Dr Elias ni nani, kapitia yapi katika maisha yake kijamii, kiuongozi na mengineyo?
Dr Elias alizaliwa tarehe 10/10/1987 (miaka 27) katika kitongoji cha Ndobo, kijiji cha Kasyabone katika kata ya Kisegese iliyopo katika jimbo Rungwe Mashariki-Busokelo
Dr Elias alisoma shule ya Msingi Nbobo 1996-2002 iliyopo wilayani Rungwe na
2003 alijiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ntaba (W. Rungwe) na kuhitimu masomo yake mwaka 2006.
Mwenyenzi Mungu hakumtupa kijana huyu akabahatika kufaulu vinzuri na kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita mwaka
2007-2009 katika shule ya Sekondari Karatu wilayani Karatu - Arusha alikosomea masomo ya sayansi yaani Biologia, Fisikia na Kemia. Katika historia yake kote alikopita Kijana Elias alikuwa makini na alikuwa ni moja ya vijana waliofanikiwa katika masomo.
Ilipofika mwaka 2009 baada ya kufaulu masomo yake ya kidato cha sita alijiunga na mafunzo ya udakitari chuo Kikuku cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS). "Huku ndiko nilikokuta na Dr Elias, nilipendezwa sana na tabia zake za kupenda kujisomea, kufanya tafiti, na kujishughulisha na shughuli mbalimbali chuoni. Nilishangaa, na nilishikwa na butwaaaa! nakujiuliza nilipoona mwanafunzi wa kidato cha kwanza anaweza kuandika proposal bila hata kufundishwa hakika nilivutiwa na kupenda kujifunza kwake. Dr Elias alikuwa ni kijana asiye na dharau, alishirikiana na wanafunzi wote, wakufunzi wake hakika walimpenda kwani alikuwa ni mfano wa kuigwa.
Akafanikiwa kumaliza masomo yake 2014 na kujiunga na mafunzo kwa vitendo katika moja ya hospital ya rufaa nchini hapa"haya ni maneno ya kijana wakaribu na Dr ELIAS
Aliendelea kusema Dr Elias amekuwa kiongozi katika ngazi mbali mbali toka shule ya sekondari hadi chuo.
Dr Elias alikuwa Kiongozi wa Taaluma Shule ya Sekondari Ntaba, Aliwahi kuwa M/kiti wa Health Club (klabu ya Afya) Shule ya Sekondari Karatu,
M/kiti wa komitii ya Utafiti ya umoja wa wanafunzi wa Udaktari (SCOMER) - Standing Commitee for Medical Education and Research.
M/kiti wa Umoja wa wanafunzi wa Udaktari (TAMSA) MUHAS,
Alikuwa M/kiti Mwanzilishi wa Chadema Students' Organization (CHASO) kwa kishirikiana na makamanda wenzake akiwepo Dr. Kilawa(Katibu), Dr. Mpokigwa (Mhazini) na wengine wengi katika chuo cha Udaktari Muhimbili (MUHAS), Kipindi hicho kwa kushirikiana na viongozi wenzake pamoja na Mh Kaihula (mb) walifanikiwa kumualika Mh Dr Wilbroad Slaa katibu mkuu Chadema Taifa kufungua tawi (Mgeni Rasmi).
Ndani ya mwaka 2014 amefanikiwa kuwa M/kiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) jimbo la Rungwe Mashariki hadi sasa.
Kijana huyu amekuwa akishiriki mambo ya kijamii toka zamani akiwa mdogo, ameshiriki harakati za kiukombozi toka mdogo hadi sasa,
Kwa kushirikiana na wanafunzi wenzake toka chuo cha MUHAS, IMTU, na KAIRUKI, walishiriki kuwapima afya na kutoa ushauri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, walifanya zoezi hili maeneo ya Biafra 2012, pia kutoa elimu ya mambo ya jinsia na uzazi kwa wanafunzi wa sekondari ndani ya Mkoa wa Pwani.
Alishiriki katika matembezi ya kuchangia ununuaji wa jenereta kubwa kwa ajili ya Hospitali ya Magonjwa ya Saratani (Ocean Road Hospital) jijini Dar es Salaam,
Lakin pia kupitia Preventive Medicine Organization (PMO) ameshiriki kutoa elimu juu ya magonjwa ya kudumu km vile kisukari na BP kwa wakazi wa Dar es Salam, ikiwemo wafanyakazi wa Benki ya NBC tawi la Kawe-Dar na wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Mbalizi Road jijini Mbeya.
Pia 2014 alishirikiana na umoja wa wanafunzi wasabato (THISDASO) vyuoni kutoa vipimo vya afya na tiba bure kwa waumini wa Mikocheni B jijini Dar es salaam.
Sasa kachukua maamuzi sahihi kushiri ki kuliinua jimbo la Rungwe, ameamua kuchukua form ya kugombea ubunge ndani ya jimbo hilo na anaamini kabisa viatu vya Prof Mark Mwandosya ni vidogo na atayafanya makubwa zaidi katika jimbo laka endapo chama chake kitampa ridhaa.
Namnukuu
Kamanda Patrick Ole Sosopi makamu mwenyekiti BAVICHA BARA, mwenye kombati Nyeusi, akiwa na makamanda wengine, Dr Elias ni huyo mwenye kombati ya kaki kulia kwa Mh Sosopi, kamanda anayetarajia kuwa mbunge wa Isimani endapo chama kitampa ridhaa na wananchi kumchagua. Walikuwepo kata ya Kambasegela
Comments
Post a Comment