KAMANDA JESKA KISHOA AKAMATWA NA POLISI KWA SHINIKIZO LA MBUNGE WA IRAMBA MASHARIKI MH MWIGULU NCHEMBA, NI AIBU YA MWAKA KWA MKUU WA WILAYA NA NAIBU WAZIRI WA FEDHA

Ni aibu ya mwaka kwa nchi inayojinasibu kuwa ya democrasia huku mawaziri wake wanatumia vibaya dhamana zao.
Pichani ni Kamanda Jesca Kishoa akiwaambia jambo polisi

Kamanda Jesca Kishoa akiwa na makamanda wengine 


Ni ushauri wa bure kwa mawaziri wa serikali yetu inayotawala kwa sasa waache tabia za kutumia dhamana walizopewa kuminya na kukandamiza demkrasia ya nchi kwa hofu za kuondolewa madarakani. Walipaswa kufanya kazi zinazowanufaisha wananchi na wao wangeamua kama wanafaa au la?

Aibu hii imekuwa ikijitokeza sehemu nyingi za nchi yetu hasa majimbo waliyotoka mawaziri au manaibu waziri wa serikali ya ccm. Lakini je ni kwanini wajihami kwa kutumia polisi? Na ni kwanini polisi nao wakubali kutumika? Kwanini wasifuate maadili ya kazi zao.

Nasema ni aibu kwa sababu kubwa moja iliyonifanya kuandika hapa kila mmoja ajue siku ya lea kamanda wa chadema Jesca kishoa ambaye ni Mke wa Mh. David kafulila (mbunge) amekamatwa na polisi kwa shinikizo la Mwigulu Nchemba  ifahamike kuwa mpambanaji huyu ndio anatazamiwa kuwa ndio mgombea ambaye anamnyima usingizi Bw Mwigulu jimbo la Iramba, lakini swali linakuja ni kwanini ashinikize na wanaoshinikizwa kukubali?  Mwigulu ni nani hadi polisi wamtii kwa kila anachowaamuru? Kwanini mkuu wa wilaya azuie mikutano ilihali polisi wametoa kibali? Yeye ni nani katika Faifa hili?

Inasemekana leo hii ni mara ya 4 mwanadada huyu kuzuiwa kufanya mikutano yake katika jimbo la Iramba. Inasemekana  mkuu wa wilaya  ndiye anayezuia wakati polisi wametoa kibali, polisi wao wanasema tatizo sio wao Tatizo ni Mwigulu anawashinikiza wahakikishe hakuna mkutano wowote unafanywa Iramba

Ni nini anachokificha au anachokiogopa?
Anafanya haya hajawa Rais, je akipewa nchi?
Nawashsuri polisi na huyo mkuu wa wilaya waache mara moja tabia ya kumbania Jeska Kishoa kufanya harakati zake za kiukombozi bali wamwambie anayewatuma na yeye aende jimboni akafanye mikutano kama wengine.
Msema kweli hupendwa na jamii na woga kwangu ni dhambi

TAFAKARI CHUKUA HATUA NA UIKATAE CCM, UMKATAE MWIGULU NA WENZAKE WOTE.

SEMA TUMECHOKA, SASA BAAASIIIIII.....

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI