Mh. KAFULILA AFUNGUKA KUHUSU ZITTO& ESCROW

Na Shindo Kilawa
Pichani ni Mh David Kafulila Mbunge (NCCR MAGEUZI)  wa kiwa na mke wake Kamanda Jesca Kishoa Kutoka Singida baada ya kupokea zawadi. 


Leo asubuhi katika kundi la watsap la IPTL BRING BACK OUR MONEY(IBBOM) liloundwa kipindi cha sakata la Escrow na vijana wapambanaji. Mh Kafulila alipohojiwa na vijana hao ndani ya kundi hilo juu ya Zitto Zuberi Kabwe kama alimsaidia katika kampeni za mwaka 2010 jimboni kwake, kama wanavyosema wapambe wa ZZK.

Mh Kafulila akaamua kufunguka, namnukuu
"Naomba kuweka kumbukumbu sawa tu kwamba Zitto ni rafiki yangu tangu nikiwa chadema lakini haimanishi tunakubaliana kila kitu. Naudhika kuona wafuasi wake wakiandika uongo ambao hata yeye mwenyewe zitto anajua ni uongo kwamba alinisaidia kwenye kampeni"
Akaendelea kwa kusema "Ukweli wa Mungu zitto hakunisaidia hata lita ya mafuta kwenye kampeni kwasababu anazojua yeye ambazo nisingependa kumsemea. Aliahidi tu kwenye magazeti. Labda wafuasi wake wamrudie kumuuliza vizuri"

Alipoulizwa juu ya sakata la Escrow uhusika wa ZZK kama anavyojinasibu kwenye Majukwaa. Mh kafulila alisema "Kuhusu escrow nimeshasema jana kwamba Umma unajua na nimeshaeleza kwamba chanzo ni gazeti la CITIZEN. Nilichofanya ni kufuatilia chanzo hicho na kufanyia kazi na ilikuwa April2014".

TUZO YA ESCROW AlIYOIPATA MH KAFULILA YAMVURUGA ZITTO.

Imebainika wazi kwamba hatua ya zitto kupanic na kulaghai umma wa watanzania kuwa yeye ndiye aliyempa nyaraka za escrow Kafulila ilijitokeza baada ya kuona umma wa Tanzania na hasa kigoma umeonesha imani kubwa kwa Kafulila kwa namna alivyosimama bila kutetereka na kwa muda mrefu hata kutaja majina ya wahusika bila woga tofauti na yeye anaetuhumiwa kuanzisha hoja kama za mabilioni ya uswiss bila kutaja majina mpaka leo ameacha watu wakijuliza tu hawajui ni nani aliyeweka mabilion Uswiss?

Hivyo Zitto Kabwe  aliamua kulazimisha tu mpaka aonekane yeye ndio mwasisi wa hoja hiyo ilihali dunia imeshatoa tuzo kwa muhusika wa kweli Mh. Kafulila

Ukweli mara zote hujitenga na uongo, ikumbukwe wakati wa sakata hili la Escrow lilipoibuliwa na Mh Kafulila Bungeni, watu wengi walidhani kuwa Mh Kafulila amepewa bomu tu ili limlipukie apotee kisiasa, Lakini Mh Kafulila alisimama kidete bila woga, alisimama kiume.

Nakumbuka kwa mara ya kwanza baada ya yeye kuibua sakata hili Bungeni alikutana na vijana  na wazee kadhaa waliokuwa na utayari kumuunga mkono  92 Hotel alikoweza kuwaeleza undani wa sakata la Escrow alikaa kwa masaa kadhaa ilikuwa kama Lecture siku hiyo. Si vibaya nikiwataja baadhi ya vijana  waliofanikiwa kushiriki kikao hicho,kilichoratibiwa na  Ben wa Saa nane kwa kushirikiana kwa karibu na vijana wengine walikuwepo Bwana Mhere Mwita, Manawa Bukwimba, Baraka Mfilinge, Shindo Kilawa, Goliath Mfalamagoha na wengine wengi  waliokubali kulivalia njuga swala hilo bila woga na kumpa sapoti kijana huyo jasiri. Wapo waliomwita Tumbili na majina mengine mengi lakini hakujali wala hakusita kuwapigania wa Tanzania.

Mh Kafulila alifanikiwa kuwaweka sawa walioshiriki kwani kila mmoja alitoka na moyo wa ujasiri zaidi walikuwa tayari kwa lolote hali iliyopelekea hata kuprint Matishirt na kuyavaa bila woga yalisomeka "IPTL BRING BACK OUR MONEY"  na wakafanikiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kueleza sakata hilo kipindi hicho yawezekana Zitto hata alikuwa hajui kama sakata hili lingefanikiwa au hata undani alikuwa hajui kwani angekuwa alikuwa anajua angelishiriki kwa ukaribu toka mwanzo wa sakata.

Ikumbukwe Mh Kafulila alikuwa akikabiliwa na kesi mahakamani ambayo mmiliki wa IPTL Bwana Seth alikuwa amemshitaki kwa kudharisha kampuni yake,. Lakini Mh Kafulila hakujali wala kutishika na  aliendelea kuwatia moyo wapambanaji alioanza nao.
Hakika ukweli hujitenga na uongo.

"IPTL BRING BACK OUR MONEY"

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI