WABUNGE WAKIIPITISHA BAJETI YA WIZARA YA AFYA WASIRUDI MAJIMBONI HAKIKA
BIG RESULTS NOW (BRN) KWA TAFSIRI YA
MAFANIKIO MAKUBWA SASA KATIKA SEKTA YA
AFYA NCHINI TANZANIA.
Na mwandishi wako,Waziri Martine Kindole
BIG RESULTS NOW sio neno geni sana miongoni
mwetu ,tuliowengi au tulio wachache bila kujali ni
wasomi,sio wasomi ,masikini,tajiri,weusi,weupe,a
u wanawake kwa wanume.Naomba ieleweke
kwamba wanaoratibu mpango huu ,wametafsiri
neno hili kwa lugha rahisi kwamba BRN ni
“MATOKEO MAKUBWA SASA”. Neno hili
limekuwa likitumiwa sana na wanasiasa
wengi,pia hata wataalamu mbalimbali katika
sekta mbalimbali nchini, ikiwemo sekta ya afya.
Kwa ujumla wake sekta ya afya ni moja ya sekta
muhimu katika ustawi wa taifa lolote na watu
wake duniani kote, kwani afya ndio msingi thabiti
wa mtu yoyote bila kujali cheo chake au pesa
zake na ndio maana sekta muhimu kama hii
inahitaji sera thabiti zinazotekelezeka.
Katika taifa letu, kumekuwa na MWENDELEZO
WA EPISODE ambayo hubadilishwa jina kila
kukicha, ila picha kuwa ile ile mifano yake halisi
ni kama;"MKUKUTA 1&2","MPANGO WA MIAKA
MITANO (5),MPANGO WA MIAKA 25 " na
mipango mingine kedekede.Na sasa tuna huu
tena ambao umekuwa ukitangazwa sana kwa jina
la ''BIG RESULTS NOW'' (BRN) hata kabla
mipango mingine haijafanikiwa na mingine
haijamalizika.Na sina hakika kama twayafanya
haya yote sijui kwa kutumia tafiti zipi,au mtu
akiamka anasema anayoyaona yafaa.
Yawezekana waliobuni na kuratibu mpango huu
wa BIG RESULTS NOW walikuwa na nia nzuri
japo sina imani na nia yao sana.
Ukiangalia kwa makini BRN katika sekta ya afya
wameainisha kutekeleza mambo mengi sana
ambayo sitayaweka yote bayana, kwa mfano
mpango wa kuwa na Zahanati Vijiji vyote,Vituo
vya afya Kata zote ,Hospitali Wilaya zote na
kuzipa hadhi ya Rufaa hospitali za Mikoa
zinazokidhi vigezo.Sambamba na hayo yote
wameonesha kuwa walilenga kuboresha huduma
za afya kwa kuboresha mazingira ya kufanyia
kazi ili yawe rafiki kwa wagonjwa na wafanyakazi
wote.Walilenga kuboresha mazingira kwa
kuhakikisha vitendea kazi vinakuwepo vya
kutosha (uwepo wa dawa ,damu salama,maabara
safi na vifaa vyote kulingana na hadhi ya ngazi
ya kituo husika) na kuhakiksha upatikanaji wa
rasilimali watu kama vile
madaktari,wauuguzi,watalaamu wa maabara
n.k,ili zikidhi vigezo na viwango vya kimataifa
kama shirika la afya duniani (WHO) linavyoyataka
mataifa kufanya hivyo. Katika hili sina budi
kuwapongeza kwani sasa vyuo vingi vinazalisha
madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa kada
nyingine zote japo kitendawili kipo na hakuna
wakukitegua hadi sasa.
Kwa kuangalia mambo yote niliyoainisha hapo juu
nitajikita zaidi Tanzania bara( iliitwa Tanganyika
enzi za ukoloni,uhuru hadi 1964 kabla ya
Muungano) kwa sababu swala la afya si la
Muungano, Tanzania bara ina mikoa 25,wilaya
133 ,vijiji 19200 na kata elfu tatu na ushee
pamoja na mipango yote thabiti hadi sasa tuna
Hospitali 21 tu za Mkoa,86 za Wilaya,Vituo vya
afya 578 na Zahanati zisizozidi 6,000. Jiulize
mwananchi mwenzangu wa bara Je,’BRN’
inawasaidia wananchi wote au wakubwa tu?
Majibu unayo mwenyewe.
Nakukumbusha tena jambo la msingi zaidi katika
sekta ya afya,SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)
wameweka vigezo katika kila jambo kukidhi
matakwa ya wananchi wote ,shirika hili la afya
duniani linataka Daktari mmoja ahudumie
wagonjwa 1000 kwa mwaka, lakini imekuwa
kinyume katika nchi nyingi Afrika ikiwemo
Tanzania.Nchini Tanzania Daktari mmoja
anahudumia wagonjwa zaidi ya 20,000 hii ikiwa
na maana ya kwamba hatujakidhi viwango vya
Shirika la Afya Duniani mara 20 zaidi.Na hiki
ndicho kiini kikuu kilichonifanya niandike
unayoyasoma ndugu msomaji wa makala
zangu.Pamoja na uwepo wa madaktari wachache
ukilinganisha na hitaji la kimataifa bado
kumekuwa na wimbi kubwa la uwepo wa
madaktari mtaani wasio na ajira. Sasa sijui ni
ukata wa serikali? Au wameona afya sio muhimu
na kuona ni bora BVR,KURA YA MAONI na
UCHAGUZI MKUU ? lakini swali linakuja mgonjwa
atapata fursa ya kupiga kura huku anakosa wa
kumuhudumia? Mimi sijui najiuliza tu kwa
mnaojua hayo mpo.
Niliumia sana,nilisikitika sana,niliwaza na
kuwazua sana,nilitafakari sana ,nilikosa nguvu
mithili ya mtu aliyekosa chakula siku tatu
nilipokutana na kijana mwenzangu niliyesoma
naye Sekondari (O’LEVEL) na alikuwa ana uwezo
mkubwa kitaaluma darasani ni balaa, (Tulimwita
shetani au Genius),Nilipomuuliza mbona upo tu
mtaani na umepungua sana mkuu?ukumbuke mi
namiliki usafiri wangu na nyumba yangu kwakuwa
familia yangu ilikuwa ni yenye uwezo
kidogo,kwahiyo sikupata shida toka nasoma hivyo
niliaza na masihala ya shuleni hapa na pale, sikia
majibu yake sasa “Asiyesikia la mkuu ……
mmmmh, ndugu yangu ni stori ndefu sana,
nilipomaliza kidato cha sita nilishauriwa na wengi
sana,ndugu na jamaa zangu,waliniambia
nikasome hata socialogy tu au education au
faculty yoyote ya miaka mitatu nikaona
wananipotezea muda nikawapuuza tu
sikuwasikiliza, kama unavyojua mtu wangu
ukionja radha ya sayansi unahisi wa
tofauti.Nakumbuka hata nilipokuwa O’ LEVEL
wewe ni miongoni mwa walionishauri nikasome
HGK au HKL ,au yoyote ile, ila sio sayansi
nikawaona hamfikirii,sasa kama unavyoona ndugu
yangu mguu wangu umeota tende, japo
mvumilivu hula mbivu lakini kwangu imekuwa
kinyume”
Duuuuh vipi mbona unanititisha kuna nini
kimekukuta au ulifukuzwa chuo?
Nilimuuliza,Akanijibu kwa upole huku machozi
yakibubujika “Nilisoma kwa juhudi sana wewe ni
shahidi toka umefahamiana nami ,nimesoma
miaka mitano chuo lakini hadi sasa nipo mtaani
kama unavyoona nafanya mishe za hapa na pale
nafikiria kurudi kijijini nikalime tu,hapa
ninapoongea na wewe kuna wenzangu zaidi ya
110 tuliotakiwa kuaza Mafunzo kwa vitendo
(internship) mwenzi wa pili hatujui hatima yetu
japo ni haki yetu kisheria baada ya kumaliza
masomo yetu” Alisema walitakiwa kupata usajili
wa kuanza mafunzo hayo kuanzia tr 15/02/2015
na kufungwa tr15/04/2015, lakini kila wakifuatilia
majibu ni yale yale ya bado swala lenu
linafanyiwa kazi. Aliongeza kwa kusema wenye
pesa za kujikimu (yaani wenye uwezo wa pesa)
waliambiwa wanaweza kuandika barua kukubali
kufanya kazi bila kulipwa kwa mda wote hadi
pesa zitakapotoka (commitment letter) ili wasije
kudai baadaye, ikiwa na maana wafanye kazi
hadi Augost bila malipo.Wapo waliofanya hivyo
kwa kuwa wametoka familia kama yangu na
wapo walioshindwa kufanya hivyo,wale wenye
uwezo mdogo kama rafiki yangu wakae mtaani
toka mwaka jana 2014 walipomaliza chuo hadi
mwaka huu Augost au September pesa
itakapopatikana .Kwani anasema hadi sasa
waliishia kuandika majina na mahali wanapotaka
kwenda, waliambiwa yanakwenda HAZINA toka
trh kumi 15 feb wanaambiwa yanafanyiwa kazi
japo hawakati tamaa kufutilia na hali hii inaweza
kuleta migogoro baina yao.Nilijikuta nakosa
nguvu zaidi baada ya story yake.Ikumbukwe
wapo wanaotumia milion 10 kwa kununua mboga
tu na milion 20 sijui 40 kwa ugolo,na haya NI
MATUNDA YA ESCROW.Waziri wa afya sijui
kama anajua kuwa tunakosa wakutuhudumia
huku madaktari wanauza nyanya kariarkoo na
mitaa mingine na wengine wanakwenda kulima
mmmmh ama kweli dunia tambala bovu.Nilifikiria
zaidi na kuona hali hii itakatisha tamaa
wanaopenda masomo ya sayansi na pia
madaktari hawa hawatukua na moyo wa
kibinadamu wanapotoa huduma kwani
wakikumbuka wanayotendewa na serikali wakati
ni haki yao kisheria mmmmmmmmmmmmmmmh
Kwa maelezo hayo tunashuhudia falsafa mpya
kutoka kwa Rais Kikwete ya 'Big Results
Now' (BRN).Hii ni falsafa isiyo na mashiko hata
kidogo iliyoratibiwa na kuanzishwa kwenye
vyumba vya Ikulu ya Tanzania, eti ije kulibadili
Taifa kwa haraka sana!!!! Sitaki kuwa msemaji
mkuu,ila tunashuhudia kweli Taifa likibadilishwa
kwa haraka sana na hiyo falsafa ya 'BRN'.Taifa
ndani ya miaka miwili limebadilika sana kwa
mfano katika sekta afya ukilinganisha bajeti ya
mwaka 2013/2014 ambayo ilikuwa ni Tsh bilioni
753 katika hii Tsh billion 282 ni matumizi ya
kawaida, na bajeti ya mwaka wa fedha
2014/2015 ambayo imepungua na kufikia Tsh
bilioni 622 katika hii matumizi ya kawaida ni
billion 317.Kumbuka malengo niliyoainisha kule
juu na yanayowakuta wasomi wa kada hii,kwa
mantiki hii moja kwa moja utaona BRN ilivyo
tamu kwa wakubwa na chungu kwa
wananchi.Jiulize kwa mapungufu ya bajeti hii
kuna uwezekano wa kuyatekeleza maswala
yaliyoainishwa na ikumbukwe nimeweka baadhi
tu.Vitu vingi vinaenda hovyo hovyo kwa kutumia
falsafa ya 'Big Results Now' iliyoasisiwa na Rais
Kikwete kupitia washauri wake.Jambo la
kujifunza ni kwamba matokeo ya hiyo 'BRN'
hayako mbali na tutashuhudia mengi katika sekta
zote nchini,kwani sijaeleza adha ya damu salamu
miezi michache iliyopita,kwani kalamu imeisha
wino nitaleta part 2 na nyinginezo muone uozo
kwenye sekta mbalimbali leo nimejikta sekta ya
afya.
Mimi kama mwanaharakati namtaka Mh.Rais,
Prof.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete aelewe kwamba
falsafa ya 'BRN' ni kula fedha za umma kifisadi
na kuharibu kizazi ambacho kinatengenezwa na
hiyo 'BRN' na hakuna lingine.Narudia tutashudia
mSengi sana ndani ya taifa hili lenye utajiri
mkubwa kama Mh hataona umuhimu wakulifanyia
kazi na mawaziri wote kwa nafasi zao na
watendaji wengine wa serikali.
USITAFUTE MCHAWI TEKELEZA MAJUKUMU
YAKO
NAJENGA TANZANIA kwa kusema ukweli
CYBERCRIME USINIGUSE kwa maslahi ya
wananchi

Comments
Post a Comment