SHEIKH MKUU MUFTI ISSA BIN SHAABAN SIMBA AFARIKI DUNIA



Mufti, Shekh mkuu  Tanzania Issa Bin Shaabani Simba enzi za Uhai wake. 

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Issa Bin Shaaban Simba amefariki asubuhi ya kuamkia leo majira ya saa nne kasorobo., Inasemekana kaaga dunia katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaamu alikokuwa akipatiwa matibabu.


Huu ni msiba mkubwa kwa watanzania wote kwani alikuwa ni nguzo kubwa katika kudumisha amani ya nchi yetu. Mwenyenzi Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu Sheikh Mkuu, Mufti Issa Bin Shaabani Simba. Na awape nguvu waislamu wote nchini Tanzania na ulimwengu mzima kwa kufikwa na msiba huu wa kuondokewa na kiongozi wao mkuu. R. I. P

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI