MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA AFARIKI DUNIA, BUNGE LASITISHWA
TAARIFA ZA KUSIKITISHA ZASITISHA BUNGE HADI TAREHE 04/06/2015
Taarifa za msiba uliotokea leo zimekuwa zakushitua na kusikitisha sana, ni za majoznzi kwa familia, wabunge, wanaukonga na wa Tanzania kwa ujumla. Imekuwa ni ghafla sana kwa hili kutokea. Hakika tufuate maandiko matakatifu yanayotueleza "kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa....."
Kwa taarifa za awali zilizotufikia hadi sasa ni kwamba Mbunge wa Ukonga jijini Dsm Mh Eugen Mwaiposa afariki dunia leo.
Inasemekana Kifo cha Mh Mama Mwaiposa kimefahamika leo asubuhi majira ya saa 4 asubuhi,. Japo haijafahamika vema kama alikuwa anaumwa au la? Lakini taarifa za awali zinasema Mh Mwaiposa amefia ndani ya Rock Hotel iliyopo jirani na kituo cha mafuta cha mabasi ya Shabiby.
Inasemekana Mh Alifika hotelini na alilala akiwa hana tatizo walipoona haamki basi wahudumu waliita polisi na kuvunja mlango ndipo wakakuta kashatangulia mbele za haki. Haijafahamika kama kafa kawaida au kwa njia nyingine ila naamini kwa umakini wa jeshi la polisi kwa upande wa utawala swala hili litafanyiwa uchunguzi wa kina na tutajua undani, tutaendelea kuwapasha habari
Mwenyenzi Mungu ailaze mahala pema roho ya Marehemu Ameni
Pichani ni Mh Mwaiposa enzi za uhai wake. R. I. P

R. I. P
ReplyDelete