Mh.KAFULILA AWALIPUA MAWAZIRI UFISADI MABEHEWA, ALITAKA BUNGE KUWAJIBISHA VIGOGO UFISADI WA MABEHEWA

Na Shindo Kilawa
Pichani ni Mh KAFULILA 


Awali mapema asbh aliomba mwongozo ripoti ya uchunguzi kuhusu ufisadi wa 238bn za ununuzi mabehewa feki iletwe lakn spika kapangua anasema kamati ndio ina haki ya kuleta bungeni na sio mbunge.

Kwa mujibu wa Kafulila wakati akichangia mara ya pili alisema ufisadi huu unahusu wizara ya uchukuzi na wizara ya fedha. Hivyo mwakyembe, katibu mkuu, waziri fedha na katibu mkuu fedha wote wanahusika kwani mlipaji mkuu ni wizara ya fedha sasa inawezekanaje malipo yafanyike kabla ya mabehewa kuletwa kama sio ufisadi.

Alihoji zaidi kwann Spika hataki serikali ilete ripoti hiyo bungeni ili mbivu na mbichi zijulikane au kwasababu ni kipindi cha lala salama imebaki kila waziri anakwapua tu wizarani kwake?.Nasisitiza ripoti ya wizi huu ni lazma iletwe bungeni ili bunge lijadili na kuamua. Hamuwezi kudanganya watu kwamba mnaongeza kodi kwenye mafuta ili mpate pesa za miradi ya umeme wakati kuna zaidi ya 238bn zinapotea.. ripoti ya PPRA ipo wazi kwamba kampuni ya India ya Hindustan ilipewa zabuni bila kufanya uchunguzi wa uwezo na weledi wa kampuni hii, kwamba wizara ya fedha ilifanya malipo yote kabla ya mabehewa kuletwa. Na mbaya zaidi mabehewa yaloletwa ni feki. Sasa kwann serikali iendelee kuficha? Kwann bunge nalo linajinyima meno kuchukulia hatua watu hawa?

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI