BUNGE LIMEKULA MATAPISHI YA ESCROW

BUNGE LIMEKULA MATAPISHI YA ESCROW

Leo kwa mara ya kwanza wabunge wa ccm wameshangilia waziri wa nishati kukanyaga maazimio ya Bunge kuhusu ESCROW.

Iliibuka baada ya mwasisi wa hoja mhe Kafulila  iliyompatia tuzo kwa kusimama bila kuyumba

Mhe kafululila alihoji kwann serikali iendelee kumlipa singasinga tozo ya uwekezaji dola 2.6m( bilioni5) kama gharama ya uwekezaji kila mweza sawa na 60bn kwa mwaka kwa muda usiojulikana.

Kafulila alihoji uhalali wa malipo hayo ilhali azimio la bunge ni mitambo hiyo kutaifishwa na zaidi ripoti ya cag ilibainisha wazi kuwa singasinga huyo manunuzi aliyafanya kwa nyaraka za kugushi ambayo ni jinai achilia mbali wizi wa pesa.

Simbachawene alijibu kuwa serikali haiwezi kutekeleza azimio hilo la bunge kwa hoja kuwa serikali itashtakiwa. Na wabunge wa ccm kumshangilia huku wakimzomea kafulila utadhani hayakuwa mazimio ya bunge.

Kafulila alisimama na kusisitiza kuwa kiti cha spika kuanzia makinda na hata zungu wamekuwa wakimdhibiti kuhakikisha hawaelezi bunge ni lini ripoti ya utekelezaji wa maazimio itawasilishwa bungeni

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI