OMBWE LA AJALI ZA BARABARANI LAIBUKA TENA MKOANI IRINGA
Ni muonekano wa gari ubavuni baada ya kupata ajali eneo hilo la kinyanambo, Mafinga
Kama unavyoona katika picha hizi, hivi ndivyo gari lilivyosambaratishwa baada ya ajali iliyoleta maumivu makali na kuacha majuzi kwa taifa letu.
Pichani ni Muonekano wa Gari aina ya Coaster la Another G baada ya kupata ajali eneo hilo la Kinyanambo, nje kidogo ya mji wa Mafinga wilayani Mfindi
Katika ajali iliyotokea usiku wa jana japo eneo la Kinyanambo,Mafinga wilayani Mfindi katika barabara kuu nje kidogo ya Mji wa Mafinga. Imeripotiwa
Kuwa watu 23 wamepoteza maisha na wengine 34 kujeruhiwa vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema gari aina ya costa mali ya Another G inayofanya safari zake kati ya mikoa ya Iringa na Njombe ilikuwa ikitokea Iringa mjini kuelekea Njombe iligongana na lori la mizigo na kusababisha maafa hayo.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Mufindi Miss. Mboni Mhita amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa hii ni miongoni mwa ajali mbaya kutokea wilayani Mufindi. Akikumbushia ajali iliyotokea mienzi michache iliyopita kutokana na uwepo wa mashimo barabarani, uzembe wa madreva na mwendo kasi, ajali hoyo ilihusisha gari la mizigo na basi kubwa la kampuni ya Majinja. Amesisitiza madreva kuwa makini, na abiria wawe wanachukua hatua madreva wakiwa wanaendesho mwendo kasi kinyume na sheria
Mwenyenzi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema na awaponye walioumia. AMEN
Comments
Post a Comment