KAFULILA: JK KAVUNJA MISINGI YA UCHUMI ALOWEKA MKAPA.

Na Mh Kafulila

Huu ndio mchango wangu bungeni jioni leo.Mkapa aliweka misingi ya uchumi mkuu( macro economics) kilichopaswa kufanywa na JK ni kuhakikisha mafanikio hayo yanajitokeza kwenye uchumi wa kawaida ili kila mtanzania aone fahari ya kukua kwa uchumi wake lakn bahati mbaya amebomoa kabisa na sasa inabidi UKAWA tuanze upya baada ya uchaguzi Oct.

1. Mkapa amepokea nchi mwaka 1995  ukuaji wa uchumi ukiwa 4.2 akakuza mpaka 6.7 mwaka 2004. Leo JK kashusha uchumi mpaka 6.4 mwaka 2014.

2. Amepokea nchi riba ya mabenki ikiwa 30-26% mwaka 1995 lakn mwaka 2005 riba za mabenki ilishuka hadi 14% lakn leo JK riba zimepanda mpaka 18%. Hii inathiri sana ukuaji wa sekta binafsi na biashara nchini.

3.Mwaka 1995 mfumko wa bei ulikuwa 21% lakn mwaka 2005 mfumko ulishuka mpaka 4%. Leo JK mfumko wa bei ni 5.3% . 

4. Mkapa kapewa nchi mwaka 1995 akiba ya fedha za kigeni zikiwa za miezi 2 lakn mwaka 2005 akiba ilikuwa ya miezi 8 lakn leo mwaka 2015 akiba za pesa za kigeni zinatosha miezi4 tu.

5. Mkapa amepewa  nchi ikiwa haikopesheki 1995 lakn mwaka 2005 deni la Taifa lilikuwa 10trilioni. Leo miaka10 JK deni limefika trilioni35 . Ziada ya 25 trilioni na kilichofanywa na deni cha maana hakionekani kwani deni hili ilipaswa tuoneshwe reli ya kati imejengwa na bandari zote za mtwara, dar, kigoma, mwanza na Tanga.lakn ni bahati mbaya deni hili sehemu kubwa ni matumizi ya kawaida kwani makusanyo ya ndani hayatoshi hata matumizi ya kawaida. Tunakopa mpaka pesa za kuendesha ofisi na mishahara.

6. Mkapa ameacha nchi ikiwa inakusanya mapato ya ndani zaidi ya asilimia14 ya pato la Taifa mwaka 2005 . Leo tunakusanya kodi sawa na asilimia 12% ya pato la Taifa.

Hii inathibitisha wazi kwamba tunapiga hatua mbili mbele na tunarudi hatua kumi nyuma kisha tunajipongeza.

Serikali inaongeza kodi ya mafuta kwa hoja kwamba tunataka pesa za umeme vijijini, nikweli tunahitaji umeme vijijini hata jimboni kwangu Nguruka, na jimbo kwa ujumla lakn ukweli ni kwamba vyanzo vingi vya fedha serikali imegoma kukusanya. Kwa mfano;

1. Tangu mwaka 2007 serikali imegoma kununua mtambo wa kurekodi matumizi ya simu ili iwe na uhakika wa mapato ya kampuni hizi. Matokeo yake kampuni hizi zinavuna trilions of shilings lakini tunapata kodi kiduchu kwasababu hakuna uhakika wa mapato ya kampuni hizi. Na hata sheria ya mawasiliono ya 2009 ilotaka ndani ya miaka3 kampuni zote ziwe zimeorodhesha hisa zao soko la mtaji DSE ili mapato na matumizi yafahamike na umma uweze kuwa sehemu ya ya wamiliki bado serikali imeshindwa kutengeneza kanuni za kutekeleza sheria iyo mpaka leo. Afu wanakuja hapa wanalazimisha kuongoza kodi ya mafuta itayoumiza raia wengi nchini

2. Kodi za uvuvi bahari kuu bado tatizo. Nchi ya namibia ukanda wake wa bahari kuu ni karibu sawa na Tz. Wao ni 1500km sisi ni 1424km.. Namibia ukiacha madini uvuvi wa eneo hii ndio chanzo cha pili cha mapato sisi tunacha meli zinavua bila kodi.

3. Mgodi wa mwadui upo tangu mwaka 1944. Na tangu uhuru hawalipi kodi kwa kutangaza hasara lakn hawaendi kwao. 

Hali ya nchi mbaya sana;
1. Leo tz ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye misitu mikubwa ya mbao afrika lakn bado tunaupungufu wa madawati 1,170,000. hii ni kwa mujibu wa taarifa ya HAKI ELIMU.  Kama kila dawati wanakaa wanafunzi3 maana yake tuna zaidi ya watoto 3milioni wanakaa chini. Hii ni aibu kwani wenzetu wa kenya sasa wanatatua tatizo la kila mwanafunzi kuwa na laptop yake. 

2. Hali ni mbaya sana kwani hata kwa mujibu wa ripoti ya USAID ya Mei2015 bado 34% ya watanzania wanaishi chini ya mstari wa umaskini.( ni fukara).

3. Na kibaya zaidi ni elimu tunayozidi kuiua. Kwani kwa mujibu wa ripoti ya USAID ya Dec2014 asilimia 70% ya watoto wanaohitimu elimu ya msingi hawajui kusoma kiswahili na 90% hawajui kusoma kingereza.

Hii ni dunia ya soko huria. Ni dunia ya ushindani. Tunahitaji rais ambae atatengeneza watanzania weledi na wenye juhudi ili hata gas na madini visipokuwepo wataishi hata nchi ikigeuka jangwa. Sasa tunazalisha binadamu wasio na maarifa wala juhudi na hili ni janga katika dunia ya ushindani. Nimetembea kidogo na kujifunza. Tofauti kubwa kati yetu na waliotuzidi ni hiyo. Binadamu wenye nidhamu ya kazi na maarifa. 

Natambua namna ilivyo changamoto kwa chumi changa katika soko huria iliyojaa makampuni makubwa. Chukua mfano mapato ya kampuni ya gas ya Statoil ambayo mapato yake 2012 tu ilikuwa ni dola 108bilion. Sasa mabos wake wanapokaa na viongozi wa serikali ndogo kama ya kwetu ambayo mapato yake kwa mwaka hayafiki dola 8bn. inahitaji ujasiri mkubwa kwani rushwa na weledi ni mtihani. Tunataka rais mwenye jeuri ya kutoza kodi wafanyabiashara wakubwa na makampuni hayo badala ya kuonea wafanyakazi.

Nimekuwa nikiwambia hapa. Tanzania inaongoza kwa kutoza kodi kubwa wafanyakazi kuliko nchi zote afrika mashariki. Inatoza wastani wa 18% . Wengine walichanganya na kima cha chini cha kodi ya 11%. Wastani ni 18%. Kwani kuna wafanyakazi wanatozwa kodi 30%. Nchi ya rwanda wastani wa kodi ya mshahara ni 5.6%, Kenya 6.8% , burundi 10.3 %na uganda 11%. Hii ni aibu kwa nchi ambayo chama tawala asili yake ni harakati za wafanyakazi masikini kutoza kodi kubwa kuliko vyama vya Kenya ambavyo asili yake ni wafanyabiashara.

Leo serikali inahadaa hata wazee kwamba ina nia ya kuwasaidia na kwamba inatunga sheria ya kuhakikisha wanalipwa mafao. Ukweli ni hadaa kwani sera ya wazee ilitungwa tangu 2006, kiutaratibu ilipaswa sheria ifuate mara moja baada ya sera. Lakn haikufanyika hivyo mpaka leo mwaka wa mwisho ndio sheria inaletwa

Naomba kusisitiza kwamba nchi hii tunaishi umasikini ambao hatukustahili. tunashinikizwa umasikini. Tunahitaji uongozi wenye kutambua hilo na ujasiri wa kukusanya mapato kukabili umasikini. Sio hii style ya kila waziri kutaka kuwa rais matokeo yake leo bajeti kuu inajadiliwa inahusu wizara zote lakn kuna mawaziri watatu tu. Jenesta, saada na Nagu. Hii ni aibu.

MUNGU UTUNUSURU NA UTAWALA HUU TENA!

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI