UKISTAAJABU YA WANAWAKE WA ROMBO UTAYAONA YA WIZARA YA UCHUKUZI NA STESHENI YA RELI MOSHI MJINI.

Na Mwl. Denis Bongole
Hili ni Daraja la Tsavo nchini kenya, ujenzi wa mradi huu unaendelea hadi sasa

Hapa ni Stesheni ya Gari moshi iliyopo mkoani Kilimanjaro, Moshi

Wiki chache zilizopita gazeti la mwananchi linalomilikiwa na kampuni ya Mwananchi communication limited lilimnukuu mkuu wa wilaya ya rombo akisema kua eti "wanawake wa rombo wanakodi wanaume wakenya kutoa huduma za kindoa"

Binafsi sikuona ajabu sana ila nilitafsiri kama 'vita ya kisiasa' dhidi ya mbunge aliepo sasa ndugu Joseph Selasini. Nilipata kuandika hapa juu ya hili hivyo leo nataka tuunganishe matukio katika sakata la aina yake ndani ya wizara ya uchukuzi.

Majuzi hapa Raisi wa Kenya bwana Uhuru Kenyata aliandika katika ukurasa wake wa facebook kuhusu safari yake na mawaziri kadhaa ambapo walionekana katika picha wakiwa wametembelea "daraja la tsavo" kukagua ujenzi wa reli ya kisasa kabisa nchini humo.

Cha ajabu zaidi ni mwaka mmoja tu toka achaguliwe ambapo pamoja na misukosuko ya kisiasa anayoandamwa nayo kuhusu ICC na sakata la al sha baab ameweza kusimamia na ujenzi unaendelea kwa kasi kukamilisha mradi huo muhimu kwa uchumi wa Kenya.

Kwetu pamoja na kua na fursa kubwa za kibiashara lakini pia amani na uvumilivu wa kisiasa, rasilimali chungu nzima bado tumeshindwa kuendeleza reli ya kaskazini na sasa pamegeuzwa kua kambi ya kufuga mbuzi na makaazi ya vibaka.

Pamoja na jitihada za mheshmiwa raisi katika kutuwekea mawaziri hodari katika wizara ya uchukuzi kama Dr. Mwakiembe na sasa mzee wa kasi na viwango bado wanaona hata aibu kufanya ziara stesheni ya reli Moshi kujionea hali ilivyo.

Sijajua sababu hasa ni nini lakini ni aibu kwa taifa na fedheha kwa watanzania kwani kufa kwa miradi hii muhimu kumeathiri mambo mengi sana hasa suala la ajira n.k

Wenzetu kenya wanasonga kwa kasi kubwa sana watanzania sijui nani afikiri kwa niaba yetu

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI