LEO NI SIKU YA KIHISTORIA KUANZA HATUA NYINGINE YA KUMALIZA DHULUMA YA KISIASA VISIWANI ZANZIBAR

Naangalia Star Tv,

Leo ni siku ya kihistoria kuanza hatua nyingine ya kumaliza dhuluma ya kisiasa visiwani Zanzibar

Na Ben Saa Nane

Maalim Seif Shariff Hamad anatangazwa leo kuwa Mgombea Urais wa Chama cha CUF mshirika Mwenza wa UKAWA  katika kinyang'anyiro cha Urais wa Zanzibar

Issa Bin Nasser katika kitabu chake "Zanzibar:Kinyang'anyiro na Utumwa" aliandika maneno haya "Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye yote na ndiye atakayemua na kuhukumu kwa haki" .Ni baada ya kuichambua dhuluma ambayo Zanzibar na wazanzibar wamekua wakifanyiwa

Maalim Seif Shariff na Chama chake cha CUF wamekua mstari wa mbele kupambana na Dhuluma hii

Binafsi katika ukuaji wangu kisiasa nimekua nikimhusudu sana Maalim Seif Sharif Hammad kwa misimamo mikali na uzalendo wa kile anachopigania kuhusu Zanzibar na Watu wake

Ni mwanamapinduzi asiyeyumbishwa

Wanasiasa wa aina hii ni nadra sana na kadiri nilivyozidi kuzama ndani na kukomaa kisiasa nilikuja kugundua ni kwanini mtu kama Maalim Seif hawezi kukaa ndani ya vyama vyenye viongozi wababaishaji na akabaki Salama na misimamo yake mikali. Ni aidha ukubaliane nao na uwe ndio mzee kwa ku-compromise principle zako au Ufukuzwe ikiwa utashindwa kuwabadilisha na kupindua Status Quo.

Maalim Seif kufukuzwa ndani ya CCM mwaka 1988 na kisha kuwekwa kizuizini kwangu mimi hainishangazi. Ameipigania Denokrasia,ameipigania Zanzibar.Zanzibar iliboresha katiba yake mwaka 2010 na kupata ahueni ya kisiasa

Raila Odinga ana kitu hiki kinachofanana na Maalim Seif na amepitia misukosuko hiyo hiyo ndani ya Vyama.Amepambana ndani ya KANU, Ndani ya FORD na nje ya Vyama Hivyo.Kenya Ilipata katiba mpya iliyofungua ukurasa mpya

Ni misimamo mikali iliyosahihi pekee inayoweza kuwakomesha madikteta kwenye vyama,taasisi na ndani ya Serikali za Kiafrika

Maalim Seif,Msomi wa Shahada ya Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ni mzoefu wa mapambano,asiyeyumbishwa vitani.Ni mvumilivu wa misukosuko lakini dhamira yake hushinda woga wake vitani

Bila shaka Kaka na mwalimu wangu kisiasa Ismail Jussa Ladhu amejifunza mengi kutoka kwa mkongwe huyu Maalim Seif Shariff

Hatua ya kuelekea Uhuru wa Kweli na haki kwa Wazanzibar imeanza Rasmi

Namtakia kila la Kheri Maalim Seif Shariff Hamad

Chini ya Rais wa UKAWA ,Wazanzibar wataweza kutamka

"Zanzibar ni Njema,Atakaye na Aje"

The brighter futere of Zanzibar is Unfolding.

Aluta Continua ,Victory Ascerta....

Ben Saanane

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI