MAANA HALISI YA USHOGA KATIKA SIASA. Wapendwa wasomaji wa makala zangu kwanza kabisa niaze kwa salamu, shikamoni wakubwa, habari za leo na hamjambo mlio wadogo kwangu. Ni tumaini langu mu wazima huku mkiendelea kushangilia umasikini tulionao. Awali ya yote ningependa kutoa ufafanuzi kidogo juu ya ushoga japo niliwahi kuandika andiko la kufanana na hili mwaka wa jana mwenzi wa kumi na moja, wengi walikimbilia kutukana tu bila kuangalia maudhui ya andiko nilichokiandiko ndicho kinachoendelea hivi sasa inshallah tuachane na hayo. Nisikuchoshe usinichosha"Ushoga"una maana kuu mbili nijuavyo mm na wachache au wengi wetu. Maana ya kwanza ushoga ni tabia ya mwanaume kuingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwenzake yaani mwanaume kuingizwa uume na mwanaume mwenzake kwenye tundu la kutolea haja kubwa (kinyesi) . Hali hii humfanya mtu anayeingizwa kujikuta kuhitaji mara kwa mara kutokana na muwasho anaoupata siku chache baada ya tendo hilo chafu na ovu, kwani wadudu/bacteria...
NA RUSTON MSANGI. Adui ni kiumbe au mtu anayemtendea mwingine uovu, kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu. Uovu unaweza kuwa wa moja kwa moja au hata kwa njia ya kutotimiza majukumu vizuri. Chama cha walimu Tanzania CWT, ni miongoni mwa vyama vya wafanyakazi nchini, kinachoshughulika na walimu. Kwa mujibu wa katiba ya CWT, pamoja na madhumuni mengi ya chama hiki, jukumu kubwa na la pekee ni kusimamia hadhi, haki na maslahi ya walimu kitaaluma, kiuchumi, kijamii nk. Ni ukweli usiopingika kwamba ni vigumu kwa mwalimu mmojammoja kujitetea lakini kupitia umoja au taasisi ya CWT inakuwa rahisi zaidi. Kauli mbiu ya CWT ni HAKI na WAJIBU. Kwa miaka mingi kinachoangaliwa ni WAJIBU huku HAKI ikiwa imezikwa na kuachiwa kila mmoja kujitetea. CWT inaendeshwa kwa pesa za wanachama wake ambao ni walimu, kwa makato ya 2% ya mshahara kila mwisho wa mwezi. Hivyo kama ni rasilimali fedha ipo ya kutosha kufanya kazi kwa maslahi ya walimu. Nitakupa mfano kiduchu wa mapato ya CW...
NA RUSTON MSANGI. Kila mfanyakazi anapoajiriwa huwa kuna utaratibu maalumu wa malipo, yaani mshahara kwa mwezi au vyovyote vile kutokana na mkataba wa kazi. Mbali na malipo ya mshahara katika ajira, pia huwa kuna namna tofautitofauti ya kuwapatia fedha ya ziada wafanyakazi wa eneo au taasisi fulani ili kuongeza morali ya ufanyaji kazi, kupunguza makali ya maisha, kufidia muda wa ziada katika kazi nk. Hii fedha hujulikana kama posho. Posho hii inaweza kutolewa kwa mwezi, siku, saa nk. Posho huweza kuwa kwa ajili ya chakula, usafiri, malazi, utendaji au namna yoyote ili itakavyokuwa imepangwa na mwajiri kwa makubaliano maalumu. Watumishi nchini Tanzania katika serikali na mashirika binafsi wanapokea posho kutokana na majukumu Yao. Kwa mfano, madaktari na polisi. Kwa upande wa walimu kwa muda mrefu imekuwa ni tofauti sana kuhusiana na suala la posho, japokuwa mwalimu mbali na jukumu kubwa na muhimu la kufundisha, hufanya kazi nyingi nyingine akiwa...
Comments
Post a Comment