Mh EDWARD NGOYAI LOWASSA NI MSAFI



Na Dr. Shindo Kilawa

Mh Edward Lowassa  akiwa ameshika fomu ya kuwania urais kupitia Chadema

Watu wengi wataishangaa kauli yangu, watakaa midomo wazi na kujiuliza maswali kibao moja ya maswali watakayojiuliza ni kama yafuatayo.

Anasema EL ni msafi wakati alithubutu kumuita Fisadi?

Usafi wake uko wapi au kwa kuwa kahamia Chadema?

Huyu anayesema haya ni mamluki au Chadema kweli?

Hayo ni baadhi tu ya maswali japo najua kuna maswali mengine mengi zaidi juu ya mh EL.

Wanapoendelea kujiuliza ni vyema na mm niwaulize maswali kadhaa kama ifuatavyo?

Kama EL ni mwizi au fisadi ni kwanini hadi leo hajakamatwa na kupelekwa Mahakamani?

Je hajakamatwa kwakuwa serikali ni dhaifu au haijui sheria inazosimamia yenyewe au iliogopa kuumbuliwa zaidi?

Toka 2008 hadi leo nini kimefanyika baada ya EL kwa kulinda heshima yake na kuamua kujiweka pembeni?

Tunadhani ni kwanini jina lake liliishia njiani? papo hapo jiulize kwanini Rizone alitweete akionesha hayupo tayari kuona Rais akitokea kaskazini kipindi cha Uhai wake?

Je ni kwanini Rais JK hajawahi kuthubutu kumsema EL hadharani?

Je ni kwanini Upinzani walimpiga sana mitandaoni na hata majukwaani lakini leo wapo meza moja?

Ni kwanini CCM walimuamini tena 2010 akapeperusha Bendera yao jimbo la Monduli? utamuaminije Mwizi?

Je ni nchi gani upinzani ilishawahi kuing'oa serikali bila kutumia watu waliokuwepo au waliopo Madarakani?

Je tunapenda kuendelea kuwa masikin kwa mfumo uliopo?

Bado nina maswali ambayo sitayamaliza sasa hivi ila endelea na ww kujihoji na kujipa majibu huku ukiangazia mfumo mzima wa chama cha mapinduzi na serikali yake ndipo utapata majibu.

Narudia kusema "EL si Mchafu hata kidogo"  lakini katika yote Mfumo wa CCM ndio mchafu na ndio unaowafanya wachafuke hata wasio wachafu, yawezekana kabisa msielewe dhana yangu lakini pia mkanielewa dhana yangu.

Mimi kama mwanachama wa chadema sipo tayari kuendelea kuitwa mpinzani lakini nipo tayari kuona nchi hii ikiwa upinzani kwa masilahi mapana ya watz  wote.

Nitaeleza kwa kina nikitulia sehemu yenye upepo mwanana

Jiunge na Team ya Ushindi
Dr. Kilawa

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI