ELIMU BURE NA CHANGAMOTO HASI.. SERIKALI ITAZAME UPYA MPANGO HUU!!

TATIZO ninaloliona nchini kwetu baada ya uchaguzi kumalizika hadi sasa miezi 7 baada ya serikali ya Rais Magufuli kuapishwa ni kuwa kuna watu wengi tunaimani na MAGUFULI..


Labda kwa kuwa anaonyesha utofauti mkubwa wa kiutendaji na watangulizi wake wengine waliopita, ni HAKI YAKE SISI kumuunga mkono, maana ni Rais wa Nchi yetu ya Tanzania.


Lakini tatizo linakuja kwa wachache wenye imani kubwa kupita kiasi, kufikia hatua ya chochote anachokosolewa (Magufuli) yeye na serikali yake, wao wanafikiri ni kuwa watu wanamtafutia ubaya au hawapendi afanikiwe.... laah! Hasha..


SIYO KWELI.


Rais Magufuli akiharibikiwa na sisi pia tumeharibikiwa maana ndiye kiongozi mkuu wa nchi yetu.., ndiye mwenye kubeba dira na matakwa ya watanzania..


Mfano mdogo sana ambao mimi binafsi mwanzoni mwa mwaka huu niliupigia kelele sana; hii 'issue' ya Elimu bure..


January mwaka huu kama ilivyotangazwa na ofisi ya Rais baadaye wizara ya elimu, kwamba wanafunzi wapate elinu yao bure.. kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, bila kutoa mchango wowote..


Hii ilileta mkanganyiko mkubwa sana, maana kuna baadhi ya shule wazazi waliombwa pesa na mahitaji makubwa sana ili wapokelewe na kuanza masomo.., tena shule hizo zikiwa ni shule za serikali..


Nikafikia hatua ya kujihoji.. hii ni ELIMU BURE au ELIMU BILA MALIPO YA ADA??


Watu ambao wanafikiri kila anaehoji hivi ni mpinzani basi wanakosea sana..


Kinywa kinachoweza kuuliza ni muhimu kuliko kile kichwa ambacho kitatumika katika kuharibu baada ya mambo kuwa yameharibika..


Maana Suala la Elimu halina itikadi,.. halina mrengo wa kisiasa na siyo la chama cha siasa... serikali itazame mchanganuo wa Elimu bure..


Changamoto nyingine katika utekelezaji wa mpango wa elimu bure ni bajeti ya mahitaji kuwa kubwa kuliko kiwango cha fedha zilizotolewa na serikali kwenda shuleni kwa ajili ya kukidhi mahitaji...


Miundombinu ya vyoo, maabara, nyumba za walimu, usaili kupata walimu wenye sifa na vigezo, ni vitu ambavyo vinapaswa kufanyiwa kazi ili mpango wa elimu bure utimie..


Pia changamoto nyingine zinazokabili mpango huu wa elimu bure ni pamoja na wanafunzi kukaa chini, uhaba wa walimu wa sayansi, vitabu vya kiada na ziada, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, baadhi ya masomo kufutwa na kupunguza baadhi ya mitihani.


Changamoto ya wanafunzi kukaa chini ni uzembe mkubwa wa serikali kuu na serikali za mitaa.. ni aibu kubwa sana kwa karne hii ya 21, miaka 54 baada ya uhuru, wanafunzi kukaa chini au juu ya mawe wakati wakipata huduma ya elimu..


Elimu bure.. imeongeza kiasi cha wanafunzi waliongia shule.., katika utaratibu maalum wa ujifunzaji, chumba cha darasa kinapaswa kuwa na wanafunzi kati ya 25-30 ili uhawilishaji wa taaluma uwe sawia kutoka kwa mwalimu kwenda kwa mwanafunzi... sasa hivi darasa moja lina wanafunzi 60-80.. hatari hii..


Katika kudhibiti tatizo la wanafunzi kuanza na kumaliza shule pasipo kujua kusoma na kuandika.., serikali ilikuja na muundo mpya wa ufundishaji maarufublama "muhamo wa ruhaza" ambao ulilenga kusaidia kudhibiti tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika... tatizo ni kwamba, walimu hawana ujuzi wa mpango huo na hawakupelekwa kwenye mafunzo kwa ajili ya kujifunza stadi hizo..


Katika uchunguzi wangu nilibaini.. kwamba, mitihani kadhaa imefutwa katika shule nyingi ili kuendana na kubana matumizi ya pesa zinazopelekwa na serikali kwenye akaunti za shule...


Kuna afisa elimu mmoja niliwahi kumsikia akisema kwamba, kuwapo kwa changamoto katika suala la elimu zimetokana na sera hiyo kuanzishwa katikati ya mwaka wa fedha hivyo hakukuwa na fedha zilizokuwa zimetengwa katika bajeti...


Kisheria mabadiliko ya bajeti katika halmashauri yanatakiwa yaidhinishwe na Baraza la Madiwani.. kumbuka mabaraza yalikuwa yamevunjwa kupisha uchaguzi mkuu, sasa jaribu kutambua changamoto walizokutana nazo maafisa elimu, waratibu elimu na walimu wakuu katika kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais kwenye maeneo yao..


Natambua.. nafahamu kwamba, sasa Dunia na wakazi wake wameathirika sana na utandawazi.. ila ni vyema kama taifa.. tukabuni mbinu mbadala za kuweza kutengeneza mazingira ya utolewaji wa elimu yetu.. mfano; nyumba za walimu hazipo.. na zilizopo hazina ubora na utimamu.. na pia, hazina hata staha ya kumweka mtumishi wa umma ili aweze kutoa huduma yake kwa staha..


kuna urasimu mkubwa sana umeanza kutokea katika taasisi za Elimu huko....


Mazingira ya utolewaji wa elimu hiyo ya bure, zana za kufundishia na kujifunzia, walimu, muktadha wa utolewaji elimu hiyo, uboreshaji wa mtaala, na pia serikali itazame namna mpya ya kutoa ithibati kwa vitabu vya kuada na ziada..


Nimeona danadana inayoendelea katika kile kinachoitwa maslahi ya wamiliki wa shule Binafsi katika kupinga utekelezaji wa agizo la Rais kuhusu bei elekezo ya ada kwa shule binafsi..


Pia jana nimemsikia naibu waziri wa elimu, akijibu swali la mmoja wa wabunge kuhusu bei elekezi ya ada kwenye shule za binafsi..


Ni wazi serikali imeamua kuegemea upande wa wawekezaji katika tasnia ya elimu.., serikali haisimami miguu yote kwa ajili ya kuleta usawa wa ufundishaji katika shule za serikali na binafsi..


Majibu ya naibu waziri wa elimu jana haya kujitosheleza, alisema serikali haiko tayari pia kuwaumiza wawekezaji.. siyo sawa hii..


Ni swala ambalo liko wazi kwamba.. elimu itolewayo kwenye shule za binafsi ni
kubwa na imara kuliko elimu kutoka shule za serikali..


Kuzungumzia ubure wa elimu umekaaje lakini wapokeaji hawapendi ukosolewaji wa Serikali ya sasa, sasa sijui mnadhani kuna serikali ya umalaika.


Kila ambaye atampinga Magufuli katika eneo fulani ataonekana ni mpinzani..


Siyo Kweli..


Mpaka sasa elimu bure imekaa kisiasa bado kiutendaji haijajidhihirisha... kuna matatizo na changamoto nyingi sana katika utekelezaji wa elimu bure..


Ingawa naungana na serikali katika kusema... Elimi burw ni moja kati ya vitu muhimu kutoka kwa serikali kwenda kwa wananchi wake.. ipangwe vyema ili isiwe na makando kando.., itekelezeke....


KULIJADILI HAKUNA UBAYA, na kutofautiana ni sehemu ya KUJENGANA... nimefikiri hivyo!!


Martin Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida,
+255719715520

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI