BAJETI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI 2016/2017

Na Mh Jacob

 Pichani: Mh Boniface Jacob,  Mstahiki meya wa Kinondoni


halmashauri ya manispaa ya kinondoni, inatarajia kutumia fedha kiasi cha Tsh billioni 248,477,433,909.00,ambapo katika fedha hizo billioni 170,489,953,899,00 ni kutoka serikali kuu,sawa na asilimia 68.6%,TSH Billioni 1,420,000,000,00 michango ya wananchi,sawa na asilimia 0.6%,Tsh Billioni 64,285,690,000,00 sawa na asilimia 25.8%,ni mapato ya ndani,huku Tsh Billioni 12,281,790,010,00  Nikitoka mfuko wa Barbara sawa na asilimia 5%,hivyo kufanya kuwa na jumla ya bajeti ya Tsh Billioni 248,477,433,909,00 katika fedha hizo  kiasi cha Tsh billioni 125,899,275,355,00 ni matumizi ya kawaida na mishahara ya watumishi,ambapo nisawa na asilimia 51% ya bajeti yote,na Tsh Billioni 122,578,158,554,00 ni fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 49%
Bajeti ya kiasi cha Tsh billioni 248,477,433,909,00 2016/2017 kutoka kwa ile ya mwaka Jana ya Tsh billioni 156,024,051,000,00 2015/2016  ni sawa na ongezeko la asilimia 59%
 MCHANGANUO WA FEDHA ZA MISHAHARA NA MATUMIZI YA KAWAIDA(Tsh billioni 125,899,275,355,00)
1.19,402,653,555,00 ni matumizi ya kawaida (O.C)
2.106,496,621,800,00

MCHANGANUO WA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO(Tsh billioni 122,578,158,554,00)
1.44,8883,036,445,00(makusanyo ya ndani)
2.76,275,122,109(kutoka serikali kuu)
3.1,420,000,000,00(machango wa wananchi)

MATUMIZI YA MAPATO YA NDANI YA TSH BILLIONI 64,285,690,000,00
1.44,883,036,445,00(Miradi ya Maendeleo) sawa na asilimia 68%
2.17,348,493,555,00(matumiziya kawaida) sawa na 28%
3.2,054,160,000,00 sawa na  asilimia 3%

MCHANGANUO WA FEDHA KUTOKA SERIKALI KUU TSH BILLIONI 170,489,953,899,00 ikiwa ni 100%
1.97,326,482,800,00 mishahara ya watumishi
2.9,170,139,000,00 matumizi ya kawaida
3.775,743,000,00 ni fidia ya vya Manispaa, vilivyo futwa na serikali kuu
4.63,993,332,099,00 fedha za miradi ya Maendeleo kutoka serikali kuu
5.12,281,790,010,00 ni ruzuku kutoka mfuko wa matengenezo ya Barbara.

BAJETI HII IMETOA VIPAUMBELE 11 2016/2017
1.UJENZI NA BARABARA
(a)kiasi cha shillingi Billioni 5.5 kimetengwa kwa ajili ya Barbara,mtaro na madaraja
(b)ununuzi wa mota greda moja,Tsh million 600
(c)kijiko kimoja cha kuchimba mitaro Tsh million 150

2.USAFISHAJI TAKA NGUMU NA MAJI.
(a) Kutenga kiasi cha Tsh BILLIONI 2.28 kwa ajili ya ununuzi wa MAROLI 25 (roli moja kila kata) ya kusombea takataka mitaani
(b)Ununuzi wa gari mbili za kusaga na kubeba takataka(compactors) Tsh BILLIONI 1.2
(c) Utengeji wa fedha kwa madeni ya makandarasi wa kubeba takataka ni Billioni 1.8
(d)Uchangiaji wa uanzishwaji wa dampo la kisasa Mabwepande

3.AFYA
(a)Tiba bure kwa wazee,kuanzia Julai mosi,wazee 1000 kila kata(1000×34=34000)
(b)Tiba bure kwa wananchi kinondoni, kwa HOSPITALI zote kubwa NNE,mwananyamala, Tandale,magomeni,na Sinza palestina,na zahanati zote 16,kwa bima ya 40,000 kila MTU kwa mwaka mzima.TIKA(Tiba kwa kadi)
(c)Ununuzi wa Magari ya wagonjwa kwa zahanati na HOSPITALI ZOTE
(d)fedha za ukarabati wa HOSPITALI na zahanati zote za manispaa ya kinondoni,pamoja na kuongeza sehemu za kujifungulia akina Mama,(TIBA YA MAMA NA MTOTO)

4.KILIMO5,MIFUGO MJINI
(b) ujenzi wa machinjio ya kisasa,mfano wa kuigwa Africa mashariki huko,Mabwepande,Tsh BILLIONI 1.4

5.MAENDELEO YA JAMII
(a) tumetenga tena fedha za mikopo ya wanawake na vijana, Tsh billioni 5.5

6.UTAWALA NA UONGOZI Tsh BILLIONI 3.1
(a) Tumepandisha posho za wenyeviti serikali za mitaa,kutoka Tsh50,000/=(hamsini elfu) mpaka kiasi cha Tsh 100,000/= (laki moja)kila mmoja
(b) posho za wajumbe serikali za mitaa,kutoka Tsh 5000/=(elfu tano kwa mwezi) mpaka 30,000/=(elfu thelathini)
(c)Fedha kwa ajili ya shajala(stationaries) na kodi,ofisi,Umeme kwa mitaa yote,(PAMOJA NA KUZUIA TOZO LA HUDUMA SERIKALI ZA MITAA KWA MIHURI)
(d) KUFUTWA MICHANGO YA MWENGE KWA WANANCHI,kwa manispaa ya kinondoni kwa wananchi wetu,kwa kutengea mwenge fedha za manispaa tuh,kiasi cha Tsh million 176.

7.MASOKO,WAMACHINGA NA BIASHARA
(a)kiasi cha Tsh Billioni 1.65
kukarabati masoko yote 23 pamoja na kuweza mazingira rafiki ya wamachinga katika masoko holela ya ubungo,Mwenge,Tegeta,Kimara stop over,manzese,na Mbezi mwishowe

8.ELIMU
(a) billioni 3 za matengenezo ya madawati 30,000,kwa sekondari na shule za msingi,kukidhi hitaji la upungufu wa madawati 28,000,ili kuacha watoto kukaa chini
(b)kutenga Tsh Billioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa. Vyoo vya shule za misimgi na kufidia machango iliyofutwa na Elimu bure
(c) kutengenezwa fedha za umaliziaji wa shule ya kidato cha tano na sita,wasichana Mabwepande(MABWE GIRL'S)
(d) uanzishwaji wa shule ya wavulana goba,(GOBA BOYS)
(e) manunuzi ya vifaa vya maabara kiasi cha Tsh  millioni 250

9.MIPANGO MIJI
(a) kupanga mji wa mfano kwa kata ya mbwenina mitaa baadhi ya kata za kawe,na kunduchi,pamoja na utunzaji wa maeneo ya wazi,barabara na uwekaji wa taa za barabarani.
(b) urasimishaji wa maeneo ya makazi holela (squater) kwa kata za manzese,Tandale,mwananyamala, kijitonyama,mabibo na kigogo
(c)Ufunguaji wa njia,mitaro na utwaji wa maeneo ya wazi yaliyomilikiwa kinyume na Sheria.

10.KUIMARISHA UKUSANYAJI WA MAPATO YA HALMASHAURI
 kutumia vyanzo vilivyopo 46,kuhakikisha vinakusanywa ipasavyo,kwa kubana mianya ya ukwapuaji wa fedha za umma,na sambamba na uimarishaji mifumo ya ukusanyaji kwa njia ya kieletroniki.
Kwa kuanzia mafanikio ya kupanda ukusanyaji,kutoka Tsh BILLIONI 46, kwa mwaka 2015/2016 mpaka Tsh BILLIONI 64 kwa mwaka 2016/2017

11.MICHEZO NA UTAMADUNI
(a)kusimamia na kuimarisha timu ya soka,ya manispaa,kutoka daraja la kwanza kwenda ligi kuu kwa msimu wa 2016/2017 kiasi cha Tsh million 200,kimetengwa
(b)kukuza vipaji kupitia Sanaa zingine kwa "KURUHUSU VIJANA KUIMBA NA KUREKODI BURE"

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI