KATIKA UTEKELEZAJI WA AHADI, MH. ESTHER N. MATIKO AWEKEZA KWENYE TEHAMA TARIME MJINI
Mh. Ester matiko akikabidhi kumputa kwa jeshi la polisi mjini Tarime
Mh Ester Matiko mbunge wa jimbo la Tarime mjini(Chadema) akimsikiliza mpiga kura wake kwa umakini wakati akiwa katika utekelezaji wake wa majukumu ya kibunge jimboni
Mh Ester Matiko akiendelea na zoezi la kukabidhi Computer kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi na sekta mbalimbali mjini Tarime
Kutokana na Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ya kuifanya dunia kua kijiji kwa kupashana habari. Mh Esther N. Matiko ameamua kuwekeza katika TEHAMA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime. Hii ni kuifanya Tarime iendane na kasi ya Mabadiliko hayo hasa kwenye Maendeleo. Akiwa katika Ziara za kutimiza ahadi zake kwa wananchi wa Tarime Mjini Mh Matiko amekabidhi Computer (Desk top) aina ya DELL kwenye taasisi za serikali na taasisi binafsi ndani ya Tarime Mjini.
Mh Matiko ametoa Computer kwenye Kituo cha Polisi Bomani, Halmashauri ya Mji wa Tarime kitengo cha TEHAMA na Umoja wa watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino) aliowahidi kuwapatia mda wowote zenye thamani ya Tsh 1,650,000/=
Akimkabidhi Computer Mkuu wa Polisi Tarime, OCD Athumani Mkilindi amemshukuru Mh Matiko kwa msaada huo kwa kuwawezesha kufanya kazi katika mfumo utakaorahisisha utendaji wao. OCD Athumani amemwambia Mh Matiko compuetr hiyo itasaidia katika uandahaji wa majarada yanayotakiwa kufikishwa Mahakamani kwa wakati ili wananchi wapate haki zao kwa wakati.
OCD Mkilindi amemwomba Mh Matiko kuendelea kuwatetea wananchi wa Tarime mjini wakiwemo watumishi wa serikali pale anapokua kwenye kutimiza majuku yake ndani ya Bunge na nje ya Bunge. Nae Mh Matiko amehaidi kuendelea kufanya hivyo bila ubaguzi wowote kwani wananchi wa Tarime Mjini wote ni watu wake. Hii ni baada ya Mh Matiko kukagua vyoo vinavyotumiwa kituoni hapo kutokua kwenye ubora wa matumizi ya binadamu.
Zuena Mvungi ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Mjini. Nae akipokea computer kutoka kwa Mh Matiko amemwambia Mh Mbunge haijawai kutokea Tarime yeye ni wa kipekee jinsi alivyojitoa kuwatumikia wananchi wake hasa kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kile kidogo anachokipata na kujitolea. Mh Zuena amemshukuru Mh Matiko na kumwakikishia ushirikiano wa kutosha kuwatumikia wananchi wa Tarime Mjini.
Ngobai Stephen ni mkuu wa kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Mji wa Tarime, nae kwa kipekee kamshukuru Mh Mbunge kwa computer hiyo kwani ni njia moja wapo ya kufikia marengo ya Halmashauri kwenye Mfumo wa TEHAMA. Ngobai amemweleza Mh Matiko Mfumo huo utakua na Manufaa makubwa sana kwenye mfumo wa elimu Tarime kwani utatumika kufindishia Masomo ya Sayansi na kua mwarobaini wa upungufu wa Walimu wa Sayansi.
Mh Mbunge Esther N. Matiko amewasihi Halmashauri ya Mji wa Tarime (TEHAMA) kuwatumia wadau wengine wa Maendeleo ili Marengo ya mfumo huo ufikiwe japo hatua za awali tayari zimeshafanyika. Hii itasaidia kupata Maendeleo kwa kasi zaidi ndani ya Tarime Mjini.
Baada ya kukabidhi Computer hizo Mh Matiko aliungana na wakazi wa Bomani kufyeka Msitu wa Hospitali ya Bomani uliokua unaonekana kuwa tishio kwa watumiaji wa njia hiyo kuingia Hospitali ya Bomani kupitia njia ya TTC. Hi ni sehemu moja wapo ya kufanya Mji wa Tarime kuwa safi kuanzia nje ya mji mpaka ndani ya mji wa Tarime.
Tarime Yetu Mshikamano Kwa Wote
Rasirimali Zetu Kwa Maendeleo Yetu
Imetolewa Na Ofisi Ya Mbunge Tarime Mjini
Peter Magwi Michael
Katibu wa Mbunge Tarime Mjini
Comments
Post a Comment