WANACHUO 33 KATI YA 36 WA CHUO CHA UALIMU MONTESSORI MTWARA WAFANYA MAHAFALI
Akizungumza katika mahafali ya ya tano ya chuo cha ualimu Montessori kwa niaba ya mkuu wa mkoa Mtwara ,mkuu wa wilaya Mtwara Bi Fatuma Ali amewataka wazazi kutumia fursa hii adhimu iliyopo katika mkoa wa huo kwa kuwapeleka vijana wao kupata elimu na taaluma mbambali zitolewazo kwenye vyuo hivyo ili kupunguza wimbi kubwa la vijana wanao zulula mitaani pasipo kazi maalum.
Pia Bi Fatuma Alli amewashauri wahitimu hao kuwa tayari kukabiliana na changamoto mbali mbali watakazo kabiliananazo pindi watakapokuwa mtaani wakisubiria nafasi za ajira kutoka serikalini na kuwataka kufanya kazi popote pale watakapo pangiwa na serikali na kuachana na tabia zilizopitwa na wakati za kutaka kufanya kazi kwa maeneo mjini.
Naye mwakilishi wa Afisa elimu mkoa Bi Jane Lutego ambaye pia ni afisa elimu watu wazima mkoa amesema kuwa kwa upande wa elimu nchini kumekuwa nachangamoto nyingi ambazo wasipokuwa makini huenda wakajikuta hawana faida na taaluma walioipata na kuishia katika hali duni kiafya, kiuchumi na kunyanyasika na jamii husika . Akizitaja changamoto hizo ni pamoja ,hali ngumu ya utendaji kazi,uahaba na uchache wa vitendea kazi ,changamoto ya upandaji madaraja na za kijamii katika sehemu za kazi.
Hizi ni sherehe za tano tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 2010 kikitokea kijiji cha luagala wilaya ya newala ambako awali kilikuwa chuo cha walimu wa shule ya awali na ilipofikia mwaka 2009 kilihamishiwa mtwara mjini na kuwa chuo cha walimu wa shule ya msingi daraja la 3A na hadi sasa chuo kimefanikiwa kuhitimisha wanafunzi wapatao 170 na wote wamefanikiwa kupata kazi katika shule mbalmbali zikiwemo za kibinafsi na kiserikali.
Comments
Post a Comment