SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) YATANGAZA LIGI KUU YA MIKOA KUAZA KUTIMUA VUMBI HIVI KARIBUNI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limetangaza Mei 14, 2016 kuwa tarehe ya
kuanza kwa Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL)
itakayozishirkisha bingwa wa kila mkoa kutoka
katika mikoa 27 nchini.
Ligi hiyo ya mabingwa wa mikoa itachezwa
katika vituo vine nchini, ambapo mshindi wa kila
kundi atapanda moja kwa moja ligi daraja la pili
(SDL) na mshindi wa pili mwenye matokeo
mazuri kutoka kundi A, B na C.
Kundi A kituo cha (Njombe) kutakua na
mabingwa wa mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya,
Rukwa, Katavi, Dar es salaam 3, Morogoro,
Kundi B kituo cha (Morogoro) kitakua na
mabingwa wa mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi,
Dar es salaam 1, Dar es salaam 2, Tanga, na
Singida.
Kundi C kituo cha (Singida) kitakua na
mabingwa wa mikoa ya Dodoma, Arusha,
Kilimanjaro, Tabora, Kagera, Manyara, na
Njombe, huku kundi D kituo cha (Kagera) kikiwa
mabingwa wa mikao ya Geita, Mwanza,
Shinyanga, Simiyu, Mara na Kigoma.
Comments
Post a Comment