MADIWANI WAITAKA SERIKALI KUKARABATI BARABARA ZIENDAZO PEMBEZONI MWA MJI
madiwani wakifuatilia kwa makini barala la utekelezaji bajeti |
Madiwani wameitaka halmashauari kupitia idara husika
kuziangalia na kuzifanyia utaratibu wa kujenga Barabara zinazo elekea pembezoni mwa mji ili
kurahisisha hali ya usafiri kwa wananchi waishio maeneo hayo.
Wakichangia agenda ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara
katika kikaoa cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa halmashauri ya mtwara manispaa madiwani hao wameitaka Halmashuri na idara
husika kuziangalia bara bara hizo kwa jicho la tatu kwani zinamchango mkubwa
katika kuiingizia kipato halmashauri
hiyo.
Madawani hao wakiongozwa Mh Masoud Dalli,Sharifa Ndille na
Mh Bandali wamezitaja barabara hizo kuwa Barabara ya Mtwara kuelekea Naliendele
moma,mkangala,Mdenga,likombe hadi ziwani,kijiji cha mbae sehemu ambayo hutoa
mchango mkubwa wa mchanaga unaotumiwa ujenzi wa nyumba nyingi katika manispaa
ya mtwara mikindani,pia ndio barabara zituwazo kuletea nishati ya kupikia kamavile
kuni,mkaa na baadhi ya mazao.
Kwa upande wa mwandisi wa ujenzi manispaa Frances Rugemalila amesekuwa
utengenezaji na ukarabati wa miundombinu hiyo huendana na Bajeti iliyowekwa na
halmashauri katiaka mwaka husika wa
fedha na yeye kama mwandisi hutekeleza
kile halmashauri wanacho kihitaji.
Rugemalila amesema kuwa barabara nyingi
zimekuwa zikichimbika kutoakana na hali ya kimazingira iliyopo kwa hivi sasa
hasa kwa kipindi hiki cha masika na wakutaka halmashauri na madiwani kuwa na
imani naye na kuahidi kuongeza ubora katika utengeneza wa barabara ndani ya
manispaa ya mtwara mikindani.
kupitia kikao hicho madiwani wamerithia maombi ya wafanya
biashara wa mbogamboga na matunda kubadilishiwa soka la sabasaba na kiangu waliko pelekwa awali na kuelekea soka la magomeni B lililopo katika
mtaa wa magomeni.
Awali wafanya bishara hao walilazimishwa kuhama eneo la soko
kuu mjini mtwara lililopo katika ya
manispaa ya mtwara mikindani na kupelekwa soko la kiangu hali iliyopelekea
kuzuka kwa makundi baina ya wafanya biashara ambapo kundil la kwanza llikubari
soko la kiangu na kundi la pili lilienda kwenye soko la sabasaba sehemu ambayo
manispaa haitambui kuwa soko .
Hiki ni kikao cha pili cha baraza la madiwani kilichoketi na
kujadili utekelezaji masuala mbambali ya kimaendeleo katika halmshauri ya
mtwara manispa ambapo kiakao awali cha
kilikuwa januari 21 mwaka huu .
Habari Kila mtu,
ReplyDeleteMimi nina Miller Porter Private mkopo Taasisi kwa wema Kazi sifa,
millerporter102@yahoo.com Kuomba leo kama unahitaji dharura
mkopo kutoka kampuni reputable, na hali nzuri na mahusiano ya kazi,
basi unapaswa kuwasiliana na sisi kama sisi kutoa mikopo kwa
kiwango cha bei nafuu maslahi ya 3% na kazi yako na sisi
itakuwa uzoefu mzuri. Kama una nia, wasiliana
nasi kwa barua pepe: millerporter102@yahoo.com
+2349057519652
millerporter102@yahoo.com
http://millerporter102.wix.com/potterfirms
Mimi wakisubiri majibu yako mwepesi
Mr Miller Porter