WAAJIRI KATIKA TAASISI MBALIMBALI WILAYANI MTWARA WAMETAKIWA KULIPA WAFANYA KAZI WAO UJIRA KULINGANA NA KAZI WANAZO FANYA

Wamiliki na waaajiri katika taasisi mbalimbali wilayani mtwara wametakiwa kuwajali na kuthamini michango ya wafanya kazi wao kwa kuangalia kazi wanazofanya na zilingane na mishahara wanayowapatia kwa mwezi.

Akitoa wito huo katika mahafali ya wahitimu wa huduma za hotelini yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Old Boma mikindani mkuu wa wilaya mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa wafanya kazi wengi katika hoteli zilizopo mjini mtwara hawalipwi ujira mkubwa kulingana na kazi wanazofanya na kupelekea kuwepo kwa vitendo visivyo vya kimaadili katika maeneo yao ya kazi.

Bi Fatuma Alli amewataka wahitimu hao kuheshimu mikataba wanayopewa na waajiri wao kwa kuwa na nidhamu ,heshima,Busara na kuendana na maadili ya kitanzania wakiwa katika huduma zao kwa wateja na wafanya kazi wengine.

Mkuu huyo wa wilaya pia amewataka wahitimu hao kujiendeleza kielimu ili kuendana soka la ajira la hivi sasa nchini na Dunia kwa ujumla,N a kuwashauri kama vijana kuwa tayari kukabiliana na mabadiliko yaliyopo sasa hivi katika mkoa wa mtwara kunako pelekea kupanuliwa mji wa mtwara kwa kuweka mipngo ya  miaka ishirini katika utengenezaji wa mji huo kwa kuhusisha kata tisa zilizopo katika halmashauri ya mtwara na kuziingiza manispaa ya mtwara mikindani hali inayopelekea kutengwa kwa maeneo maalum kwa ajiri masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambayo vijana ndio wahusika katika maendeleo hayo.


Kwa upande wa wahitimu Lcus Navilongo ameshukuru mafunzo aliyoyapata na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kujiari na sio kutegemea ajira kutoka katika kampuni au shirika lolote hii ni kutokana na mafunzo rafiki ya kujiajiri aliyoyapta chuoni hapo na kuwataka vijana wengine kujitokeza kusoma na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana linalopelekea kuwepo kwa mrundikano wa vijana mitaa wasio na kazi




Naye meneja mradi wa TRADE AID mtwara Bw Emmanuel Mwambe amesema kuwa Trade aid ni shirika anzilishi na old boma mtwara katika kutoa elimu  mbalimbali zinazo husu huduma za hotelinikwa vijana ambapo tangu waanze mwaka 2014 wamefanikiwa kuhitimisha vijana zaidi ya 600 waliopata taaluma kupitia chuoni hapo.
Hata hivyo Bw Emma ni miongoni mwa wahitimu wa chuo hicho aliyefanikiwa kupata nafasi kuwa meneja mradi trade aid na kuwashauri wazazi na walezi kuwaleta vijana wao katika chuo hicho.
Wahitimu wa mahafali wakiwa katika picha pamoja jana katika  ukumbi wa old boma mtwara mikindani

Comments

  1. Front size is too large (maneno utazani bango la vodacom....angalieni kusona inakuwa shigidi.shidaaaaa)

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI