MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI MH BONIFACE JACOB AENDELEA KUCHANJA MBUGA KWA KASI YA AJABU ZAIDI YA MWENDO WA ROCKETI
Mh Boniface Jacob akiwa na wananch wake wakati akiendelea na ziara yake ya kuwagawia hundi za mikopo wananchi waliojiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiliamali. Hapo kama unavyoana wananchi walivyofurahi kwa pamoja na mh wao, kushoto kwa mh ni kijana wa ccm akiwa na furaha kubwa sana kutembelewa na meya wake wa kinondoni
Na kilawa the Iron
Diwani wa kata ya Ubungo ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni wa sasa Mh Boniface Jacob ameonekana kuwa na kasi ya ajabu katika utendaji wake wa kazi ya kuwatumikia wananchi wa manispaa ya kinondoni amedhihirisha kuwa ni kiongozi wa mfano wa kuigwa.
Toka alipoaza kuwatumikia wananchi wa manispaa hiyo ya kinondoni amekuwa akifanya kwa vitendo na si kwa maneno au blabla. Ni imani yangu kuwa kama mameya wa manispaa nyingine zote nchini na wenyeviti wa halmashauri zote na viongozi wengine waliopewa mamlaka ya kuongoza wananchi wakiamua kufuata nyayo za Mh. Boniface Jacob basi tutaishi kama wafalme nchini hapa. Kwa kasi hii hakika Boniface anaendelea kutuelimisha na kutubadilisha kifikira kwamba tunahitaji mabadiliko ya juu karibu nchi nzima.
Hivi karibuni mstahiki meya bwana Mh Boniface Jacob aliwatangaziwa wananchi kuwa bajeti ya mwaka 2016/2017 itawawezesha wananchi kupata huduma bure za afya pia alisema watapata mikopo itakayoweza kuwainua kiuchumi na ameonesha mikakati mbalimbali ya kuwaendeleza wananchi ili wanufaike na raslimali zao.
Juzi tr april 20, mh Boniface alifanikiwa kusaini mkataba na kampuni ya MS/H. P GAUFF INGENIEURE GMBH&CO, KG-JBB ambayo itatoa huduma za ushauri (CONSULTANT SERVICES) katika usimamizi wa ujenzi wa miradi ya DMDP(DAR-ES-SALAAM METROPOLITAN, DEVELOPMENT PROJECT) itakayotekelezwa katika manispaa ya kinondoni. Mradi huu utasaidia kupunguza au kuondoa kabisa foleni na mafuriko kinondoni hapo. Akizungumza na mwandishi wetu mh Boniface anasema"Foleni, mafuriko yatabaki kuwa historia ya manispaa ya kinondoni...... naahidi kuwatumikia wananchi wangu usiku na mchana kwa moyo wangu wote" mstahiki meya amedhamiria kuwatumikia wananchi ili wasijute kuchagu UKAWA anatamani wananchi wote wanufaike na raslimali zao.
Mstahiki meya mh Boniface Jacob akiwa ameshikilia hundi ya milioni tatu pamoja na wajasiliamali
Kulia ni Mh mbunge wa jimbo la ubungo wakipata chakula cha mchana katika mgahawa wa mama nitilie mojawapo katika vikundi walivyotembelea.
Hapa ni Mstahiki meya mh Boniface akinena jambo na hawa akina mama
Wananchi na wanakikundi walioamua kijiongezea kipato kupitia ujasiliamali wakiwa wakiwa katika picha ya pamoja mh Boniface Jacob baada ya kukabidhiwa hundi ya mikopo
Siku ya leo april 22, Mh Boniface amefanikiwa kutembelea vikundi mbalimbali katika manispaa ya kinondoni akiwa katika zoezi la kuwagawia hundi za mikopo ili wananchi hao wawezi kujikwamua kiuchumi hii ni dhahiri kuwa mh Boniface yupo tayari na anafurahia kuona wananchi wake wanajikwamua kiuchumi.
Mojawapo ya vikundi vilivyotembelewa na mstahiki meya Boniface Jacob ni
Kikundi cha akina mama wanaojishughulisha na ushonaji wa nguo, saloon na mama lishe Kigogo-Mbuyuni ambapo aliwakabidhi hundi ya milioni 7.7
Kikundi cha akina mama kinachojishughulisha na uuzaji wa samaki na mama lishe Kimara - Kilingule B ambapo amekabidhi hundi ya tsh Milioni 3
Pia alifanikiwa kufika kuungana na mbunge wa jimbo la ubungo Mh Saed Kubenea ambaye aliwasisitiza wananchi wajitekeze kwa wingi ili waweze kupata mikopo hii ya vikundi na kuwaahidi kuisukuma zaidi serikali ili iweze kuongeza fedha nyingi zaidi kwenye miradi kama hii.
Kwa mjibu wa taarifa kutoka chazo cha kuaminika Mh Meya ametembelea vituo vingi kwa wakati mfupi ambavyo sitaweza kuviorodhesha vyote hapa na pia amefanikiwa kutatua kero nyingi kwa mda mfupi.
Comments
Post a Comment