NANYAMBA YAMALIZA TATIZO LA MADAWATI KWA ASILIMIA 100%
Ongeza kichwa |
Meneja wa TTCL mkoa wa Bw Umishael Temba kushoto akimkabidhi mkuu wa wilaya mtwara Fatuma Alli moja kati ya madawati 40 |
Katika kuunga mkono agizo la Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe magufuli halmashauri mpya ya Nanyamba mkoani Mtwara imekamilisha kwa asilimia 100% utengenezaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari.
Akipokea msaada wa meza na viti 40 kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya simu Tanzania TTCL mkuu wa wilaya Mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa anashukuru kampuni hiyo kwakuona umuhimu wa elimu na kuahidi kutowaangusha katika utunzaji wa samani hizo.
Sambamba na hilo Fatuma Alli amesema kuwa meza na madawati hayo yanapekwa katika halmashauri ya Nanyamba ambako kwa idadi hiyo itamaliza tatizo la meza na madawati kwa asilimia 100% katika shule za msingi na sekondari.
Kwa upande wa maneja wa simu Tanzania TTCL mkoa wa Mtwara Mhandisi Rumishael Temba amesema kuwa wao kama kampuni ya mawasiliano ni sehemu ya jamii yenye wajibu wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo katika elimu hivyo kwa kitendo cha kukabidhi meza na viti arobaini ni katika kutimiza wajibu wao.,
pia Rumishael ameomba uongozi wa wilaya kupitia kwa mkuu wa wilaya kusaidi ulinzi katika miundombinu ya kampuni hiyo kwani wananchi wamekuwa na tabia ya kuvamia na kuharibu kunako leta hasara kubwa kiundeshaji wa kampuni
Uchongeshwaji na ukarabati wa madawati katika shule za msingi na sekondari ni agizo lililotolewa na Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuhakikisha kila halmashauri nchini kuhakikisha linaondoa tatizo la upungufu wa madawati na hadi kufikia tarehe 30/06/2016 liwe limekamilika na wanafunzi kuanza kuyatumia .
Comments
Post a Comment