VIJANA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA ILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA AJIRA
Vijana mkoani Mtwara wametakiwa kutambua fursa za kibiashara
zilizopo kwa kuwa tayari kuungana na mashirika mbalimbali yanayo wekeza na
kutoa elimu ya kibiashara hasa ya kiujasiriamali mkoani hapa.
Akizungumza katika semina fupi iliyo husisha walezi
wajasiria Mali wilayani mtwara katika ukumbi wa Naville Novell hotel mtwara
Manispaa kaimu mgeni rasmi Bw JOHANSEN K. BUKWALI ambaye pia katibu tawala
msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani mtwara amewataka vijana kutobweteka kwa
kukaa vijiweni bali wajiingize ktk vikundi vya uzalishaji mali na kuipa
kipaumbele elimu ya ujasiriamali inayotolewa na mashirika mbalimbali mkoani
humu.
Bwana Bukwali ameishukuru Taasisi ya ujasiriamali na ushindani
Tanzania (TECC)tawi la Mtwara kwa kuwawezesha vijana kupata elimu ya
ujasiliamali na kuwaomba kuendelea na moyo huyo kwa kuwawezesha vijana kupata
elimu hiyo itakayo wezesha kupunguza tatizo la aajira kwa vijana na kuwakomboa
kiuchumi.
Groria Nyandindi na Abdallah Chilangala ambao ni miongoni mwa
wajasiriamali walio patiwa elimu na Taasisi hiyo wameshukuru kupata elimu ya
ujasiriamali ambayo imewaweza kubadilisha mfumo wa maisha na uchumi saidizi wa maisha yao.
Hata hivyo wajasiriamali hao wamesema kuwa changamoto kubwa
inayo wakabili ni kutokupata mikopo kwa wakati hali inayotishia kukwimisha kwa
maendeleo ya mitaji yao.
Naye mmoja wa walezi wa wajasiriamali kutoka taasisi ya ujasiriamali na ushindani Tanzania tawi la Mtwara (TECC) Bwa Mustafa Kwiyunga amesema kuwa wao kama walezi wanajukumu la kusimamia na kuwapatia vijana elimu stahiki ya kibiashara hasa ya ujasiria mali.
Taasisi ya ujasiriamali na ushindani Tanzania (TECC} ni mfuko wa
muda merefu ulioanzishwa mwaka 1984 ukiwa na lengo la kuwasaidia vijana na wanawake ili kuwawezesha kuchangamkia fursa
za kiujasiriamali ili kuweza kujiletea
maendeleo.
Comments
Post a Comment