𝐊𝐈𝐓𝐔 𝐆𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐈𝐍𝐀𝐓𝐎𝐊𝐄𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐀


Na Dr Elimina Chuma



Leo nita-share stori moja iliyotokea kipindi naanza kazi takribani miaka nane iliyopita.


Palikuwa na mama mmoja aliyekuwa na miaka 90 na alikuwa amelazwa kwa sababu ya moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri.  Tatizo hilo lililotokana na kuwa na shinikizo la juu la damu kwa miaka mingi. Wakati analetwa alikuwa amevimba miguu na alikuwa analala akiwa amekaa. Siku za mwanzoni alikuwa kwenye oksijeni lakini baadae alitolewa baada ya kupata nafuu; kila saa alikuwa anasema, “jamani nimechoka mwenzenu, nitakuja hospitali hadi lini?”


Ilipita kama wiki mbili hivi yule mama akiwa bado wodini, nakumbuka ilikuwa jumanne na nilikuwa zamu siku hiyo. Nilipita round wodini pamoja na daktari mkuu wa  hospitali ile. Yule mama alikuwa amepata nafuu sana, miguu ilikuwa imenywea, alikuwa anapumua kawaida na kila kitu chake kilikuwa kawaida. Tulipanga kumruhusu kwenda nyumbani kesho yake. Baada ya kuwaona wagonjwa wa wodini nilielekea kliniki kuona wagonjwa wa nje. Nikiwa kliniki, muda mfupi tu baada ya round,  alikuja nesi mbio mbio akiita, “Dokta, dokta, yule mama kabadilika”.  Niliinuka haraka sana kurudi wodini. Nilikuta yule mama hapumui na mapigo yake ya moyo yalikuwa yanasikika kwa mbali sana. Tulipigania maisha yake sana na baada ya muda alirudi kawaida. Alipozinduka alinishika mkono akaniambia, “Mwanangu nakushukuru, nilikuwa kwenye shimo refu kuna majitu yana nguvu yalikuwa yananivuta lakini wewe ukawa hukubali kuniachia, ulikuwa unanivuta kwa nguvu sana mpaka ukanitoa”. Mama huyu alifariki asubuhi ya siku iliyofuata, siku ambayo ilitarajiwa kwamba angetoka wodini kwa sababu alikuwa amepata nafuu kubwa sana. 


Ninamkumbuka sana kwa sababu aliniachia maswali mengi ninayojiuliza mpaka leo, je mtu akikaribia kufa anafahamu? Wakati mtu anakufa anaona vitu gani? Baada ya kufa tunakwenda wapi? 


Umewahi kusikia stori zingine za watu waliopitia matukio ya kukaribia kufa/waliokufa halafu wakarudi? Share kwenye comments.

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI