Mohamed Hamisi ni mlemavu mwenye malengo makubwa na yenye tija

Pichan:Mlemavu anayependa kujishughulisha

Pichan:Mh Ally Bananga Diwani wa kata ya Sombetini kupitia Chadema akiwa na Mohamed Hamisi ambaye ni mlemavu mwenye nia ya kujishughulisha badala ya kuishi kama omba omba wakijadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo

Mohamed Hamisi ni mkazi wa Sombetini. Ana umri wa miaka 24. Ni mtoto wa marehemu Hamisi Faustine. Ni mlemavu wa miguu na mkono mmoja pia una shida. Hapendi kuomba, anapenda kujishughulisha. Kwa sasa anafanya vikazi vidogo vidogo vya kuweka tinted kwenye magari lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa.
  Anatamani  kuwa na biashara nyingine ndogo ili aweze kuongeza kipato kuwasaidia wadogo zake watano ambapo mdogo kabisa ana miaka minne.
   Anaomba msaada afungue ofisi yake ili achanganye kazi zake ya kuweka tinted (maana sasa anafanya kwa mtu) na pia ofisi hiyo ataweza kuongeza biashara nyingine ya kuuza na kuburn VCD, kuuza mitumba vocha na kadhalika. Pia baiskeli yake ni nzito, ni ya mbao na chuma hasa ukizingatia anatumia mkono mmoja zaidi.
*Ombi langu kwenu*
Tumkopeshe mungu kupitia kijana huyu tukiamini ni jukumu letu kama jamii kumsaidia. Namba yake ni *+255768924516* inapokea M-pesa na jina la YUKI HAMISI.* Pia mnaweza kumpigia kumsikiliza zaidi.πŸ™πŸΌπŸ™πŸΌπŸ™πŸΌπŸ™πŸΌ

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

Posho hii ifike hadi kwa walimu