WOGA UNAVYOWATESA WALIMU!
NA RUSTON MSANGI.
Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu toleo la pili, 2004, Woga ni hali ya kuwa na hofu ya kufikwa na jambo la kutisha au la taabu.
Hali ya kutoweza kustahimili vitisho, hofu.
Waajiriwa wote ulimwenguni wanapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu. Wakiwa wanatimiza wajibu wao na kupata haki zao bila mateso na manyanyaso yoyote ndani na nje ya eneo la kazi.
Nchini Tanzania hali iko tofauti sana kwa wafanyakazi wengi, hususani WALIMU, ambayo ni kada pekee yenye watumishi wengi nchini.
Kwa muda mrefu sana walimu wamekuwa ni kundi pekee ambalo kila kiongozi wa nchi hii anaona ni sehemu ya kuchukulia umaarufu.
Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, viongozi wa kata, viongozi wa CCM nk, Kwa muda mrefu kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtumia Mwalimu kama sehemu ya kujaribia utendaji wao.
Manyanyaso, udhalilishaji na ukandamizwaji kwa Walimu sio kwamba walimu wanaupenda na kukubali, bali ni WOGA tu unawasumbua walimu wengi.
Matukio mengi ya kudhalilisha walimu kwa kiasi kikubwa yanachochewa na woga wa walimu kwa muda mrefu sana.
Mbali na matukio mengi kuripotiwa kutokea kipindi cha nyuma na kukemewa, lakini hadi hivi karibuni yamejitokeza matukio mengi ya ajabu kwa nyakati tofauti.
Octoba 3, 2016 iliripotiwa kutokea tukio la kinyama mkoani Arusha, ambapo mwalimu Batuli wa shule ya msingi Unga Ltd alitekwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili kwa njama za mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Bwana Athuman Kihamia kwa kushirikiana na Mbunge wa viti maalumu (CCM) Catherane Magige.
Mnano tarehe 17 Octoba 2016, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke alimuamuru mwalimu Hamis Sengo wa shule ya sekondari kudeki darasa mbele ya wanafunzi.
Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima toleo la Octoba 28, 2016 siku ya Ijumaa, limeripoti kuhusu mkurugenzi huyu huyu wa Misungwi Bwana Eliud ambapo anatuhumiwa kuwaamuru walimu watano (5) wa sekondari ya Ntulya kudeki vyoo vya shule.
Mwezi huu huu Octoba tumeshuhudia tukio la kustaajabisha pale ambapo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Bwana Msukuma alipoamuru kumshusha cheo cha ualimu mkuu, Mwalimu Denis Otieno wa shule ya sekondari Kasamwa. Kosa kubwa likiwa kusimamia kanuni, taratibu na sheria za shule, ambapo maslahi ya CCM yalisiginwa.
Matukio haya ya mfano yamejitokeza ndani ya kipindi kifupi katika mwezi wa Octoba 2016 pekee. Lakini kichocheo kikubwa kikiwa ni woga wa walimu, woga unaruhusu mengi sana kutokea.
Waga wa walimu wengi nchini unatokana na mambo kadhaa yafuatayo,-
Mosi, walimu wengi wana hofu na ajira walizonazo, yaani wanaamini wako kwenye ajira kwa bahati tu. Hii inachochea woga sana.
Mbili, walimu wengi hawajui sheria, kanuni na taratibu juu ya haki zao katika eneo la kazi kwa ujumla.
Tatu, Kukosa mtetezi rasmi wa kweli katika kutetea walimu na kusimamia haki za walimu. CWT imeonekana kupwaya.
Nne, baadhi ya walimu wanaamini kwamba viongozi wa Halmashauri na serikali kwa ujumla wako juu ya sheria, hivyo wana haki ya kufanya lolote kwa walimu hata kama ni kinyume cha sheria.
Tano, Baadhi ya walimu inaelezwa kuwa vyeti vyao sio vya halali, hii huwafanya kuwa na woga wa kupitiliza.
Kwa namna moja au nyingine hizi ni baadhi ya sababu za woga kwa walimu katika kutekeleza majukumu yao, ambapo kupitia woga, walimu hudhalilika na kudhalilisha taaluma zao na vyuo walivyosoma.
Ili kuondokana na hali hii ya woga usio na sababu, ni muhimu mambo yafuatayo kufanyiwa kazi,-
Mosi, walimu wawe na umoja na ushirikiano wenyewe kwa wenyewe ndani na nje ya eneo la kazi. Hali hii itachochea upendo na mshikamano ambapo walimu hawatakuwa tayari kunyamaza pale mwenzao atakapoonewa.
Mbili, walimu ni muhimu sana kuzisoma sheria, kanuni na taratibu za kazi na kuzielewa vizuri. Hii itasaidia kujua pale haki zinakapokiukwa kwa kwenda kinyume na taratibu.
Tatu, walimu wanatakiwa kupinga aina yoyote ya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki utakaotendwa na kiongzoi yeyote katika eneo la kazi. Mfano, Mwalimu unaambiwa deki darasa, na wewe unadeki. Huu ni upuuzi.
Nne, Chama cha walimu nchini C.W.T kinapaswa kuamka kutoka usingizini na kufanya kazi ya kutetea walimu. Mojawapo ya dhumuni la CWT ni kutetea haki za walimu.
Tano, serikali ichukue hatua stahiki kwa watendaji wake wote wanaoripotiwa kufanya vitendo vya ukiukwaji wa haki na kinyume kabisa na mikataba ya kazi kwa walimu.
Ukimya wa serikali katika hali hii unachochea vurugu na madhara yake ni makubwa kwa vizazi vya leo na baadae.
Mwalimu yeyote nchini anayetendewa kitendo kibaya, akakikubali na kunyamaza basi ujue ameridhika na woga ndicho kichocheo kikuu.
Imefika wakati sasa kwa walimu kuweka woga pembeni, woga ni adui wa haki, woga ni chanzo cha manyanyaso, woga hudhalilisha utu na maarifa.
Hata vitabu vya dini vimesisitiza watu kuondokana na woga usio na sababu yoyote ile kwenye maisha.
Hivyo nawaasa walimu wote nchini, fanyeni kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za kazi huku mkitimiza wajibu na kudai haki zenu, lakini woga weka pembeni, haufai na haulipi.
Mwandishi ni mchambuzi wa masuala ya Elimu.
Namba yake ya simu:0684 731516
Barua pepe:rustonmsangi@yahoo.com

Comments
Post a Comment