UZALENDO WA KWELI HAUNA MIPAKA.

.
Na, Emmanuel Chengula,


Uzalendo ni hali ya kupenda, kuamini, ama pengne kukihusudu kitu fulani kutoka moyoni bila kuwa na mazingira ya kukulazimisha kufanya hivyo.

Uzalendo ni zaidi ya love affection, ni zaidi ya mashart ni zaidi ya shinikizo na una kawaida ya kutenda haki na pengine kutoa uhai wa watu au mtu ili kitu hicho kisalimike.

Duniani kote kuna mgawanyiko wa watu wenye baadhi ya dondoo za uzalendo lakini sio wazalendo kama lilivo neno lenyewe lakin pia wachache walihesabika ni wazalendo kama mwl nyerere, Nkwame nkrumah, steve bikko, Nelson Mandela, Marcus Gurvey, Martin Luther Jr, Indra Gandhi n.k.

Kwa kawaida uzalendo wa kweli ni ule unaoangalia nchi kwa ujumla pamoja na watu wake japo kuwa kuna watu ambao wameugawa uzalendo na kuegemea kwenye chombo ama kitu kimoja; mfano kuna wazalendo wa vyama vya siasa, dini, serikali tu, bunge tu, mahakama tu, haki za wanyonge tu matajiri hana uzalendo nao, matajiri tu maskini hataki hata kuwasikia, wenye ufahamu mzuri tu, wenye ufahamu mbovu tu, haya yote yanafanyika kulingana na mahali ulipo na pengne mtu angepewa nafasi kubwa ya kiuongozi angeweza kusimama katikati ya msingi halisi wa uzalendo. Japo kuwa uzalendo uliokuwa mkuu kuliko wote ni kulipenda taifa lako ambalo unaliishi.

Lakini sasa napenda kuufafanua uzalendo wenye uwezo wa kupelekea kujengeka kwa taifa imara dunian na likawa mfano kwa mataifa mengne na huo ndo msingi sahihi wa uzalendo.

*Moja na kigezo kikuu cha uzalendo ni kutimiza wajibu na majukumu ambayo mtu amepewa ayafanye* na pengine kuyaboresha pale alipopangiwa ama kuzidi pale alipopangiwa ili asiharibu maana sahihi ya majukumu hayo.

Mfano unapokua mwl basi fundisha sana maana hukuenda kusoma ualimu kwa sababu serikali ilikua inatoa mkopo kwa asilimia 100 kwa fani hiyo ili hali fani zingine zikinyimwa mkopo na pengne kupata kidogo.

Nakumbuka miaka ya 90 ilikua kila mmoja ukimuuliza unataka kuwa nani angelikuambia nataka kuwa mwl kwasababu nyerere alikua mwl na alionyesha uzalendo pasna kubagua watu kwa kabila zao, imani ya vyama vyao na pengne elimu zao.

Unapokua mwanasheria jaji, hakimu uzalendo ni kutekeleza mambo yale ambayo sheria imesema na pengne kutumia hekima kubwa na busara na katika maamuzi yako hakikisha "a reasonable man" hatoki akiwa na mashaka na maamuzi uliyoyatoa kwamba pale jamaa kala rushwa, pale jamaa ni ndugu yake pale jamaa kafanya vile kwasababu wamesoma wote, uzalendo ni kusimama katikati na kusema hii ni _nyeusi na hii ni nyeupe".

Vivyo hivyo unapokua askar uzalendo ni kufanya na kufuata sheria zinazokupa nguvu ya kufanya jambo lolote ikiwa ni pamoja na kufuata amri halali za wakubwa wako na si vingnevyo.

Nakumbuka _ukisoma sheria moja wapo ya jeshi la polisi inaitwa " the police force and auxiliary force Act  sambamba na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai(the criminal procedure Act Cap 20 R.E 2002) inasema " _a police is the only organ which has powers inter alia to conduct investigation of
 crimes against any person suspected to have committed crimes in Tanzania"

Yaan kwa tafsri nyepesi ni kwamba polisi ni chombo pekee chenye nguvu pamoja na mambo mengine kufanya uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyofanywa na mtuhumiwa wa makosa hayo Tanzania".

Kwa mantiki hiyo uzalendo utajikita katika kazi hiyo mfano juz juzi C.P Simoni Siro(kamanda kanda maalumu ya Dar es Salaam) walipata taarifa ya kuwa kuna watu ni majambazi wapo wanne lakn wakati wakiendelea na operation kwa mujb wa sheria wakamkuta bwana mmoja anaechapisha(kugushi) nyaraka mbali mbali za serikali yaani vyeti vya darasa la saba, kidato cha  4 cha sita, vyuo, lesen mbalimbali, na kwa bahati nzuri jamaa anasema ana majina ya wote waliochukua vyeti hivyo.

Hapa uzalendo ambao tunategemea kuuona katika jeshi la polisi ni kukamata wale wote wanahusika na kugushi sambamba na polisi wenyewe kama  wapo, mawaziri kama wapo na wenye vyeo vikubwa kwani ni ukweli usiopingika wenye uwezo wengi ndio wanaweza gharimia upatikanaji wa vyeti feki kuliko maskini wa kajujumeli, igoda na kwingneko.

Kwa hiyo pamoja na kwamba mara kadha askari wanakutana na mgogoro wa nafsi/sheria kwamba wakikuta mfano mkubwa wao ndo mwenye cheti feki je watamkamata? Kwa mujb wa kanuni za asili yaani (principles of natural justices hasa rule aginst bias(no one who can be a judge on his own cause) hazitaki wajichunguze wenyewe maana huwa kuna uwezekano mkubwa mtu kuyojisemea maovu yake mwenyewe.

Hapo uzalendo ni pale polisi wanapopeleka mapendekezo ya kuundwa kwa chombo maalumu(nje ya jeshi hilo)  kitakchoshughulika na mambo kinzani hasa yanayowahusu ili kuhakikisha haki inatendeka sambamba na matukio yaliyowahi kurepotiwa Legal and human Rights centre kwenye kitabu chao cha   (human rights report ya 2014)

Uzalendo unazingatia sana haki za binadamu na kanuni za asili za utoaji haki (principles of natural justice) japo kuwa mara zingine uzalendo hugharimu maisha ya kama ilivowahi tokea nchi nyingi za africa pale wapigania uhuru walipokufa vitani wakidai uhuru kwa sababu walilipenda sana bara la Africa (they decided to choose the lesser evil) kumbe uzalendo unaotakiwa hapa ni kuhakikisha kila mtanzania anafurahia kuzaliwa ama kuishi Tanzania kwa kuangalia misingi ya haki za binadamu kama zilivyoelezwa katika ibara ya 13-30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pasipo kubaguliwa kwa itikadi zao za vyama, dini zao, makabila yao wala sehemu watokazo.

Uzalendo ni kuhakikisha Tanzania aliyowai itamani mwalimu nyerere inatimia kwa kuruhusu mawazo tofauti yanayosigana ili mwisho wa siku majibu sahihi yatoke " _ yaani ni kanuni tu dunian kote kwamba hutakiwi kujisifu kwamba nina watoto ambao nikitoka narudi hawajatoa hata betri kwenye limonti, ama hawapasua sahani hata moja ama pengine hawajauliza mama kwanini kasema tuwe tunakoleza moto bila kufunua alichopika* ila kanuni kwamba una haki ya kujivunia unapokuta katika watoto wanne mmoja kapasua sahani, mwingne  anakuhoji kwanini hufunui ulichopika, ama mbona limonti inafanya watu waonekane ama wasimame kwenye tv hivyo akaamua kutoa betri na kuona nyaya tu?

Uzalendo ni kuruhusu fikra huru zitawale katika jamii ikiwa ni pamoja na kufanya yale jamii kubwa inayoamini kwamba kwa hayo wanaamini watakuwa wametendewa haki na taifa limetendewa haki.

Uzalendo ni kuhakikisha jamii inakuwa na haki ya kupata habari sahihi kwa wakati sahihi, kutoka kwa mtu sahihi na kwa sababu sahihi ndio maana muasisi wa uzalendo alianzisha bunge likiwa linaonekana kwa jamii hiyo.

Uzalendo ni kuhesabu kwamba mimi ni baba yenu hivyo nitawapangia kazi na kuitekeleza kwa misingi na kanuni za nchi husika paspo kuathiri matakwa ya raia na mali zao.

Uzalendo katika taifa lolote duniani ni pale unapoamua kuweka chama cha siasa kando na kuhakikisha mtu anapewa nafasi kulingana na upeo, taaluma na utalaamu wa jambo husika ili naye afanye jambo hilo kwa weredi mkubwa maana ndo jambo alilolipenda  akalisomea na pengne akafanya na shughuli zingne kwaajili ya kukuza uzeofu juu ya jambo husika.

Uzalendo haufundishwi "its an inborn character" japo kuwa uzalendo huchochewa ama hupelekewa na mambo anuai ili kuboresha uzalendo huo, mambo hayo ni pamoja na;

Mishahara mizuri ya mtu huyu, makazi mazuri, kujali, utu, fadhili, uhakika wa usafiri, uhakika wa huduma mhimu kwa mazingira husuka. Hivyo vinachochea uzalendo japo haimaanish kutokuwepo kwake daktari, nesi, mwalimu, askari, mhasibu atatoroka kazini, ataacha kazi ama atachukia mfumo zaidi ya kubaki na kuamini kwamba kesho atatendewa hivyo leo ngoja afanye kwa ustawi wa taifa lake.

Uzalendo sio maigizo ya ziara mbalimbali za kushtukiza, sio matamko yasiyotekelezeka (matamko yenye nguvu siku zote ni yale ya kitaalam na siyo yale ya kisiasa) mfano daktari akisema kariakoo sokon kuna ugonjwa kipindupindu ( mlipuko) hivyo biashara zifungwe zitafungwa tu(linatekelezeka), lakini mwanasiasa akisema naona nitahakikisha kunatengwa sehem ya kunywea pombe mkoani Dar es Salaam na sehemu za makazi wakati mji huo ulishatengwa hivyo kama alivyoukuta (hili ni mfano wa agizo la kisiasa halitekelezeki).

Tanzania ni yetu sote tuipende Tanzania tuende kinyume na wahujumu uchumi, tuende kinyume na wala rushwa, twende kinyume na wavunja katiba, twende kinyume na wanaovunja sheria za nchi, tufichue waharifu, tufichue wale wote ambao wanahujumu wasomi kwa kufoji vyeti, wanaohujumu wale waliofaulu kwa sababu ya umaskini wakati wanajipanga kwenda shule matajiri wakanunua majina yao(nafasi zao) na kujikuta hawasomi pengne wanaendelea kulalamika mioyoni kimya kimya--- uzalendo ni mhimu kwa kila mtu.

Uzalendo ni kuruhusu na kuheshimu mawazo utu wa watu hata kama wachache madamu mawazo yao ni kwaajili ya lengo la kujenga nchi na si vingnevyo.

Emmanuel Chengula.
3dimension of Critical thinker

Comments

Popular posts from this blog

MAANA HALISI YA USHOGA WA KISIASA, OGOPA KAMA UKOMA, EPUKA KUTUMIKA

KILIMO CHA NYANYA

SABABU ZA WASOMI KUWA MASIKINI