UKAWA INATAKA KUSHINDA AU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU 2015?
UKAWA inataka kushinda Uchaguzi au inataka Kushiriki Uchaguzi? Yericko Nyerere Kushindwa kwa upinzani nchni kwa kiwango kikubwa katika chaguzi hizi kunatokana na muundo wa vyombo vya maamuzi ya uchaguzi wa nchi yetu, mathalani, Katiba, Tume. Kwasasa Katiba inasema kuwa matokeo ya urais hayatahojiwa na mtu yeyote ama chombo chochote wala mahali popote, hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa Tume anayechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM na anayelipwa na Mwenyekiti wa ccm akitangaza jina fulani hata kwa bahati mbaya tu baai haruhusiwi kurekebisha. Mwaka 2010 baada ya kushindwa uchaguzi mkuu, Upinzani chini ya Chadema uliituhumu sana tume Uchaguzi kwakuchakachua matokeo ambayo ilipoka ushindi wa 64% wa Dr Slaa malalamiko yao ndiyo yalipelekea kuwepo mchakato wa kuandika katiba mpya. Mchakato huo umeishia kwa zengwe la CCM kuvuruga maoni ya umma na kuweka maoni yao ambayo ni kinyume kabisa na matakwa ya umma, Maridhiano ya upinzani na msanii wa ccm baada ya dalili za uwepo finyu wa kati