Na Musa Makongoro Tayari chama cha mapinduzi kimempata, mgombea urais wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa njia za mizengwe na kupelekea mpasuko ndani ya chama hicho kuonekana hadharani. Mgombea huyu ni Dr John Pombe Maghufuli, ambaye ni waziri wa ujenzi wa serikali inayoondoka madarakani. Ni kama vile watanzania wengi, wanakubali kwamba huyu ndiye anaeweza kuirudisha nchi pale ilipokuwa na kwamba atakidhi matarajio yao. Pamoja na umahili wake wa kukariri takwimu mbalimbali, kitendo kilichomjengea umaarufu miongoni mwa watanzania wengi wasiofuatilia mambo, John Pombe Magufuri ataingia kusimamia mfumo ule ule. Tumesahau kwamba ni Magufuri huyuhuyu, ameshiriki kupitisha sheria mbovu kabisa na zenye maslahi binafsi ya baadhi ya wana CCM bungeni. Wakati bunge maalumu la katiba likiizika rasimu ya jaji waryoba, iliyokuwa imesheni maoni ya wananchi alikuwamo bungeni na hakuonyesha nia yoyote ya kutetea wananchi wa Tanzania. Rundo la kashfa zikiwemo za upotevu wa m