UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOPUNGUZA NGUVU ZA KIUME
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume. Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction). 1. Sukari. Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitish