Posts

Muuguzi mahiri kutoka hospitali ya Taifa ya Mhimbili -Mloganzila aipaisha fani ya uuguzi nchini

 Na mwandishi wetu.  Muuguzi wa hospitali ya Taifa ya Mhimbili-Mloganzola, Bw. Wilson Fungameza Gwesa  ameibuka mshindi kwa nafasi ya tano kati ya wauguzi hamsini na mbili elfu (52,000) walioshindwa  kutoka nchi zaidi ya 200 duniani. Kwa lugha nyingine amekuwa miongoni mwa wauguzi watano bora duniani. Mashindano haya ya wauguzi yaliandaliwa na Aster Guardian Nursing Award kutoka London. Kwa namna moja au nyingine Bw.Fungameza ameliwakilisha taifa na hospitali ya MNH-Mloganzila kwa umahiri mkubwa lakini pia ameipa heshima kubwa sana fani ya uuguzi nchini. Mmoja wa watumishi kutoka hospital ya Mloganzila anamesema "Wilson fungameza amekuwa ni mbunifu na anajituma sana katika kutoa huduma za kiuuguzi kwa ufanisi mkubwa sana" Bw.Fungameza ameandika kitabu katika fani ya uuguzi kinachotumika vyuoni na maeneo ya kazi ,kwa mjibu wa mtoa taarifa anasema ukisoma kitabu hicho utajifunza mambo mengi juu ya kutambua matatizo ya wagonjwa na namna ya kuwahudumia. Mbali na uandishi...

MICHIRIZI

  Utangulizi Ipo mistari inayoweza kutokea mwilini maarufu kama “mistari ya unene”. Mistari hii hutokea zaidi kwa sababu ya mabadiliko katika uzito wa mwili. Unaweza kuona mistari hii katika sehemu mbalimbali za mwili wako hasa kwenye matiti, nyonga na makalio. Mistari hii haina madhara yoyote kwa mwili lakini baadhi ya watu hawafurahii muonekano huo. Mistari hii hufifia kadri muda unavyokwenda hata bila matibabu yoyote. Una uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mistari hii kama ni: i. Mwanamke; ii. Una ndugu wenye mistari hii; iii. U mjauzito; iv. Umeongezeka uzito wa mwili kwa ghafla; v. Unapitia kipindi cha balehe; vi. Unatumia dawa za steroids vii. Misuli yako imekua kwa ghafla kwa kunyanyua vitu vizito na viii. Kama una baadhi ya magonjwa mf. "Cushing syndrome" (kwenye ugonjwa huu homoni ya cortisol inakuwa juu mwilini. Mbali na kujitokeza mistari hii, kunakuwa na dalili zingine pia kama pressure kuwa juu, mafuta kujaa zaidi kuzunguka tumbo na shingoni, ngozi kuchubuka kirahi...

𝐊𝐈𝐓𝐔 𝐆𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐈𝐍𝐀𝐓𝐎𝐊𝐄𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐀

Image
Na Dr Elimina Chuma Leo nita-share stori moja iliyotokea kipindi naanza kazi takribani miaka nane iliyopita. Palikuwa na mama mmoja aliyekuwa na miaka 90 na alikuwa amelazwa kwa sababu ya moyo wake kushindwa kufanya kazi vizuri.  Tatizo hilo lililotokana na kuwa na shinikizo la juu la damu kwa miaka mingi. Wakati analetwa alikuwa amevimba miguu na alikuwa analala akiwa amekaa. Siku za mwanzoni alikuwa kwenye oksijeni lakini baadae alitolewa baada ya kupata nafuu; kila saa alikuwa anasema, “jamani nimechoka mwenzenu, nitakuja hospitali hadi lini?” Ilipita kama wiki mbili hivi yule mama akiwa bado wodini, nakumbuka ilikuwa jumanne na nilikuwa zamu siku hiyo. Nilipita round wodini pamoja na daktari mkuu wa  hospitali ile. Yule mama alikuwa amepata nafuu sana, miguu ilikuwa imenywea, alikuwa anapumua kawaida na kila kitu chake kilikuwa kawaida. Tulipanga kumruhusu kwenda nyumbani kesho yake. Baada ya kuwaona wagonjwa wa wodini nilielekea kliniki kuona wagonjwa wa nje. Nikiwa klini...

MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Image
 Na Dr Elimina Chuma ,MD Pichani: Inaonesha jinsi  Moyo unavyofanya kazi na mgawanyo wa mishipa ya damu. Utangulizi Umewahi kuona mtu anayejisikia kuchoka sana huku amevimba tumbo na miguu, anapata tabu kufanya shughuli za kawaida mf. Kuinuka na akilala chali anaishiwa pumzi? Inawezekana moyo wake ulikuwa umeshindwa kufanya kazi kwa jinsi inavyotakiwa. Mara nyingi moyo ukishindwa kufanya kazi utahitaji matibabu kwa maisha yote ili uweze kuishi kawaida.  Kitu gani husababisha moyo kushindwa kufanya kazi? 1. Magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo; 2. Shinikizo la juu la damu; 3. Magonjwa ya valvu za moyo; 4. Magonjwa ya misuli ya moyo; 5. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo mf. Matundu kwenye moyo; 6. Mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio na 7. Magonjwa mengine sugu mf. UKIMWI na Kisukari. Unaweza kuona dalili zifuatazo kama moyo wako umeshindwa kufanya kazi: 1. Kuishiwa pumzi unapojaribu kutembea/kusimama; 2. Kushindwa kupumua ukiwa umelala; 3. Kuishiwa nguvu na kusikia kuchoka s...

𝐅𝐀𝐈𝐃𝐀 𝟓 𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐎 𝐔𝐁𝐎𝐍𝐆𝐎 𝐖𝐀𝐊𝐎 𝐔𝐍𝐀𝐏𝐀𝐓𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐙𝐎𝐄𝐙𝐈

Image
Na Dr.Elimina Chuma,MD Unapofanya mazoezi kuna kemikali na homoni mbalimbali zinazotengenezwa ambazo zina faida kubwa kwa ubongo na afya ya akili. 𝐊𝐢𝐥𝐚 𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐞𝐦𝐢𝐤𝐚𝐥𝐢/𝐡𝐨𝐦𝐨𝐧𝐢 𝐡𝐢𝐳𝐨 𝐢𝐧𝐚 𝐟𝐚𝐢𝐝𝐚 𝐳𝐚𝐤𝐞 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐢𝐟𝐮𝐚𝐭𝐚𝐯𝐲𝐨: 1. Endofini- hupunguza maumivu; 2. Serotonini- hukusaidia kujisikia vizuri kwa ujumla; 3. Dopamini- hukuchangamsha, zinakupa motisha, umakini na zinakusaidia kujifunza; 4. Norepinefrini- huongeza umakini, mtazamo na hukupa motisha na 5. Zipo homoni zingine ambazo zinasaidia kukarabati mishipa ya fahamu, kuunganisha seli mbalimbali za ubongo na kusaidia akili kufunguka zaidi. Taja faida zingine za mazoezi. #exercise #fitness #workout #gym #motivation #health #fit #training #fitnessmotivation #healthy #healthylifestyle

Je tunatibu dalili au tunatibu ugonjwa?

Image
Ugonjwa ndio unasababisha dalili.  Na Dr Cyrilo Unaweza kutibu dalili usitibu ugonjwa (na sidhani kama neno kutibu litakuwa sahihi hapo) Lakini ukitibu ugonjwa bila shaka utakuwa umeondoa dalili.  Mfano! Dalili za Malaria: homa, maumivu ya viungo, kichwa, kuchoka mwili, kutapika.... nk Sasa ukipewa dawa ya homa na maumivu, yawezekana homa na maumivu vikaoungua au kuondoka, lakini bila dawa ya kuangamiza vimelea vya Malaria bado hujatibu ugonjwa... Na kwahiyo dalili hizo zitarejea opunde... 🤷🏽‍♂️

Walimu tujitafakari katika utoaji wa adhabu, hatma yetu iko mikononi mwetu

Image
NA RUSTON MSANGI. Kuna msemo unasema  kinga ni bora kuliko tiba, yaani ni bora uwe na tahadhari ya kukabiliana au kujihami na jambo lolote na si kusubiria hadi tatizo lijitokeze. Siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio makubwa mawili nchini yanayohusisha walimu na wanafunzi. Tukio la kwanza ni la Agosti 27, 2018 ambapo mwalimu Respicius Patrick na mwenzake Herieth Gerald wa shule ya msingi Kibeta mkoani Kagera, wanatuhumiwa kwa kumuadhibu hadi kumsababishia kifo mwanafunzi wao Sperius Eradius wa darasa la tano. Chanzo cha tukio hili inasemekana ni mwanafunzi huyo kuhusishwa na wizi wa pochi ya mwalimu. Na hadi sasa walimu hawa wamesomewa mashtaka ya kuua kwa kukusudia katika kesi ya mauaji namba 18 ya mwaka 2018. Tukio lingine ni lile la mwalimu wa sekondari ya Kalangalala mkoani Geita aliyejulikana kwa jina la Rauson Lechapia anatuhumiwa kumshambulia kwa ngumi mwanafunzi wa kidato cha sita Jonathan Mkono hadi kupelekea kulazwa hospitali kutokana na maumivu makali. ...

Uchambuzi wa kifasihi katika wimbo wa Roma na Stamina uitwao Parapanda!

Image
NA RUSTON MSANGI. Fasihi ni sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira/jamii iliyokusudiwa. Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum. Nyimbo huburudisha, kuelimisha, kusifia, kuliwaza nk. Hivi karibuni msanii Roma kwa mara nyingine, na kwasasa akiwa na mwenzake Stamina wamekonga nyoyo za mashabiki wa muziki na fasihi kwa ujumla kutokana na wimbo wao maarufu wa Parapanda. Wafuatiliaji wa mashairi ya Roma kwa muda mrefu, watakubaliana nami kwamba Roma amepiga hatua kubwa sana hasa katika matumizi ya fasihi. Katika wimbo huo wasanii Roma na Stamina wamekuja na aina tofauti kabisa. Wasanii hawa wamevaa uhusika wa watu wawili maarufu kwenye historia ya taifa letu, ambao kwa sasa hatuko nao hapa duniani. Yaani Baba wa taifa Mwal. Julius Kambarage Nyerere na Kingunge Ngombare Mwiru. Roma akiwa ni Nyerere na Stamina akivaa uhusika wa mzee Kingunge. Wasanii hawa wamefanya hivi kuvuta taswira juu ya mtazamo wa watu maarufu na ...

Wakuu wa shule wapata nafasi ya kukomoa walimu.

Image
NA RUSTON MSANGI. Ni wiki kadhaa sasa walimu wengi nchini wamekuwa katika msongo wa mawazo, hii ni kutokana na agizo la serikali linalotaka walimu wa sekondari wa stashahada na shahada wanaosemekana ni wa ziada kwa masomo ya sanaa wapelekwe shule za msingi. Mapema sana nilionesha kutokukubaliana na agizo hili kwa kuwa ni kimyume na mkataba, humuathiri mwalimu kisaikolojia, humshusha mwalimu cheo, hunyima wahusika ajira, nk. Katika utekelezaji wa agizo hili ambalo limepingwa na walimu wengi wenye akili, kumezuka matatizo makubwa zaidi. Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari nchini wamepata nafasi ya kuonyesha chuki za wazi kabisa kwa walimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa namna moja au nyingine wakuu wa shule wamehusika moja kwa moja katika zoezi la kuhamisha walimu kutoka sekondari kwenda shule za msingi. Na ushiriki wa wakuu wa shule haujawa wa heri wala haki, bali imekuwa ni nafasi kwao kuadhibu, kukomoa na kuondoa watu ambao wanahisi ni kero kwao. Nayasema hay...

Adui mkubwa wa walimu ni CWT.

Image
NA RUSTON MSANGI. Adui ni kiumbe au mtu anayemtendea mwingine uovu, kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu. Uovu unaweza kuwa wa moja kwa moja au hata kwa njia ya kutotimiza majukumu vizuri. Chama cha walimu Tanzania CWT,  ni miongoni mwa vyama vya wafanyakazi nchini, kinachoshughulika na walimu. Kwa mujibu wa katiba ya CWT, pamoja na madhumuni mengi ya chama hiki, jukumu kubwa na la pekee ni kusimamia hadhi, haki na maslahi ya walimu kitaaluma, kiuchumi, kijamii nk. Ni ukweli usiopingika kwamba ni vigumu kwa mwalimu mmojammoja kujitetea lakini kupitia umoja au taasisi ya CWT inakuwa rahisi zaidi. Kauli mbiu ya CWT ni HAKI na WAJIBU. Kwa miaka mingi kinachoangaliwa ni WAJIBU huku HAKI ikiwa imezikwa na kuachiwa kila mmoja kujitetea. CWT inaendeshwa kwa pesa za wanachama wake ambao ni walimu, kwa makato ya 2% ya mshahara kila mwisho wa mwezi. Hivyo kama ni rasilimali fedha ipo ya kutosha kufanya kazi kwa maslahi ya walimu. Nitakupa mfano kiduchu wa mapato ya CW...

Mohamed Hamisi ni mlemavu mwenye malengo makubwa na yenye tija

Image
Pichan:Mlemavu anayependa kujishughulisha Pichan:Mh Ally Bananga Diwani wa kata ya Sombetini kupitia Chadema akiwa na Mohamed Hamisi ambaye ni mlemavu mwenye nia ya kujishughulisha badala ya kuishi kama omba omba wakijadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo Mohamed Hamisi ni mkazi wa Sombetini. Ana umri wa miaka 24. Ni mtoto wa marehemu Hamisi Faustine. Ni mlemavu wa miguu na mkono mmoja pia una shida. Hapendi kuomba, anapenda kujishughulisha. Kwa sasa anafanya vikazi vidogo vidogo vya kuweka tinted kwenye magari lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa.   Anatamani  kuwa na biashara nyingine ndogo ili aweze kuongeza kipato kuwasaidia wadogo zake watano ambapo mdogo kabisa ana miaka minne.    Anaomba msaada afungue ofisi yake ili achanganye kazi zake ya kuweka tinted (maana sasa anafanya kwa mtu) na pia ofisi hiyo ataweza kuongeza biashara nyingine ya kuuza na kuburn VCD, kuuza mitumba vocha na kadhalika. Pia baiskeli yake ni nzito, ni ya mbao na chuma has...

RICHARD TAMBWE HIZA KUZIKWA LEO

Image
Pichani:Ratiba ya mazishi ya Mh Richard Tambwe Hiza aliyefariki ghafla juzi asubuhi kwa tatizo la Pumu lilokuwa likimsumbua kwa Mda mrefu.

Pata vichwa vya habari katika magazeti ya leo

Image

BREAKING NEWS:MH SUGU NA MASONGA WAACHIWA HURU KWA DHAMANA

MH. SUGU NA MSONGA  WAACHIWA HURU KWA DHAMANA MUDA HUU SAA 19: 03 USIKU KATIKA MAHAKAMA YA MKOA WA MBEYA BAADA YA KESI YAO KUSIKILIZWA KWA SIKU NBILI MFULULIZO . HUKUMU ITATOLEWA TAR 26/02/2018. Leonce Marto  Mwenyekiti Bavicha Iringa mjini amethibitisha akiwa katika mahojiano mwandishi wetu Leonce Marto ametoa Shukrani za dhati kwa Wakili Kibatala na wenzake pamoja na wananchi wote wa jiji la  Mbeya

CHADEMA YAENDELEA KUCHANJA MBUGA KINONDONI HUKU MAELFU YA WANANCHI WAKIWAUNGA MKONO

Image
Pichani:Wananchi wa kata ya Magomeni waliojitokeza kwa wingi kuwasikiliza viongozi na Mgombea wa Chadema Pichan:Wanachi wa kata ya magomeni wakiwa na nyuso za furaha wakati wakisikiliza sera za mgombea wa chadema  kata ya magomeni Pichani:Mgombea wa Chadema Salum Mwalimu  akiomba kura kwa wananchi wa Kata ya Magomeni waliofurika kumsikiliza Pichani:Mh Boniface Jacob ,Mstahiki Meya wa Ubungo akimnadi Mgombea wa Chadema Ndg Salumu Mwalimu, katika  Mkutano wa Kampeni za CHADEMA uliofanyika leo Kata ya Magomeni jijini Dar Es Salaam ambapo Meya wa Ubungo Boniface Jacob alikuwa Mgeni rasmi wa Mkutano huu.