Posts

Showing posts from May, 2015

PERUZI VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO, 01/06/2015

Image

SEMA SASA BAAASIIIIII MAUAJI YA WALEMAVU WA NGOZI (ALBINO)

Image
KUKITHIRI KWA VITENDO HARAMU VYA MAUAJI YA ALBINO KWAITIKISA  TANZANIA. Na Shindo Kilawa Pichani ni baadhi ya matukio yaliyofanywa kwa wenzetu hawa wenye ulemavu wa ngozi 👉KEMEA ,PAZA SAUTI ,SEMA VIFO VYA MAALBINO SASA BAAASIIIIII KWA NGUVU👈            Kumekuwa na mtikisiko mkubwa nchini Tanzania kwa vitendo haramu na vya kikatili  vinavyoendelea ndani ya jamiii zetu kwa hawa ndugu zetu Albino.Vitendo hivi  vinaendelea kuwatia hofu wananchi wenzetu na kujikuta kama wao ni wakimbizi ndani ya nchi yao ,pia wazazi wao hawana raha kila kuchwao .Hakika inasikitisha ,inahuzunisha,inasonosha,inagadhabisha pale unaposikia au kuona katika vyombo vya habari binadamu mwenzako kakatwa viungo au kauwawa na binadamu wenzetu ,wala sio fisi wala sio  simba mmmmmmmh. Naomba tuangalie kwa kifupi maana halisi ya Albino.                    Albino ni nani? Bila shaka kila mmoja wetu neno hili sio geni sikioni kwake na hata kama hujasikia basi uliona sehemu limeandikwa.           Albino ni

MAZINGAOMBWE YA SAFARI YA MATUMAINI

Image
SAFARI YA MATUMAINI NA MAZINGAOMBWE. Na Patrick Tungu. Nimesikia wakisema "Safari ya matumaini" waliyoaza nayo leo kuelekea magogoni. Ni jambo la kushangaza sana kuendelea kuamini mazingaombwe ya watia nia kutoka CCM. Sasa najiuliza kwanini iwe ni Safari ya matumaini na sio ya uhakika, inamaani hatutafika? Nimeamua kuandika ili wananchi wengine wajue hatuhitaji safari ya matumaini tunahitaji kiongozi atakayefanya kwa vitendo katika kila sekta. Nipo arusha tangu mchana wa leo nimetokea Dodoma bungeni asubuhi lakini nilichokiona huku ni lindi la upotofu na huluka za kimaslai tu lakini pia watu wamekuja kusikia jamaa anasema nini? Japo asimilimia kubwa ya waliohudhuria wamelipwa pesa yaani wametolewa mikoani kwa gharama kubwa, ni aibu sana hata wanaojiita wasomi wa vyuo vikuu pamoja na kulia Boom lakini waliletwa pale. Eti 4U ndo nini sasa? Nilichoumia zaidi zaidi baada ya Balozi  mmoja nchi za nje alipomuinbox Aunt yangu aliyepo huko ughaibuni akimweliza pesa kubwa

PATA MAGAZETI YA LEO

Image

HAYA NAWEZA ANDIKA BAADA YA KAULI YA MKUU WA WILAYA ROMBO

Image
HAYA NAWEZA ANDIKA BAADA YA KAULI ILE YA MKUU WA WILAYA YA ROMBO Na mwl.  Denis Bongole Kuna kundi moja linaitwa ROMBO UNION ambalo kwa sasa siwezi kupata wala kuandika taarifa baada ya wenyemamlaka walinitoa ili kudhibiti sauti yangu isisikike. kabla ya taarrifa kuhusu wanawake wa rombo kuzagaa nilipata kubishana sana na wanaccmpale kwenye group ya Rombo Union kuhusu suala la kumbebesha lawama mbunge wetu bwana Joseph selasini na kadhia ya kufurika kwa pombe nyingi sana. Na nilichokielewa kwa haraka baada ya mjadala ule  sakata la ulevi ilikua ni jambo ambalo lipo kisiasa badala ya kuwaza kama jamii. Niliuliza swali jepesi sana je majukumu ya mbunge ni yapi? Na katika udhibiti wa pombe haramu nani aliepo karibu zaidi na udhibiti? Ni mbunge ambaye anapaswa kua mwakilishi wetu bungeni ama ni mkuu wa wilaya, watendaji wa kata, mkurugenzi, jeshi la polisi ama sisi raia tunaoishi pale kijijini? Nilienda mbali zaidi na kusema inakuaje waliopaswa kufunga na kupiga marufuku kabisa

UKIMYA KATIKA SEKTA YA KILIMO

Image
UKIMYA KATIKA SEKTA YA KILIMO Na Mwl. Bongole Pichani ni wakulima ambao wanapumzika baada ya kuchuma nyanya zao Si kila anayeanza safari hufika mwisho wa safari husika. Naaam japo bado tunasafiri matumaini ya kufika yapo ila si kwa siku chache. Sizungumzii kupanda daladala na kuelekea machinjioni au mahali popote pale nikiwa na maana ya mtaa ama kijiweni. La hasha!!  Nazungumzia safari katika usimamizi bora wa idara ama sekta ya kilimo ili kufikia mahali ambapo tutakua na uwezo wa kuzalisha chakula cha kututosha na kuuza nje ya nchi tena si uarabuni ama ulaya na marekani hapana tuwauzie warundi waganda na hata wasudani na wakenya ambao kwao ardhi ni kidogo. Wanunue kwetu, tuzalishe kwa ajili yao. Nilifundishwa darasani kwangu kua ukizalisha bidhaa na kuuza kwa wenzio hasa nje ya nchi utajipatia fedha za kigeni. Naam hatuna usimamizi bora katika kilimo. Sera ya kilimo na ufugaji ni nzuri sana ina kila aina ya mikakati na namna sahihi ya kufikia mapinduzi ya kilimo. Najikuta

PATA VICHWA VYA HABARI KUTOKA KATIKA MAGAZETI YA LEO

Image
PERUZI VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO

PATA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO

Image
           PERUZI MAGAZETI YA LEO HAPA Tembelea mara kwa mara blog hii, www.tujue.blogspot.com