Walimu tujitafakari katika utoaji wa adhabu, hatma yetu iko mikononi mwetu
NA RUSTON MSANGI. Kuna msemo unasema kinga ni bora kuliko tiba, yaani ni bora uwe na tahadhari ya kukabiliana au kujihami na jambo lolote na si kusubiria hadi tatizo lijitokeze. Siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio makubwa mawili nchini yanayohusisha walimu na wanafunzi. Tukio la kwanza ni la Agosti 27, 2018 ambapo mwalimu Respicius Patrick na mwenzake Herieth Gerald wa shule ya msingi Kibeta mkoani Kagera, wanatuhumiwa kwa kumuadhibu hadi kumsababishia kifo mwanafunzi wao Sperius Eradius wa darasa la tano. Chanzo cha tukio hili inasemekana ni mwanafunzi huyo kuhusishwa na wizi wa pochi ya mwalimu. Na hadi sasa walimu hawa wamesomewa mashtaka ya kuua kwa kukusudia katika kesi ya mauaji namba 18 ya mwaka 2018. Tukio lingine ni lile la mwalimu wa sekondari ya Kalangalala mkoani Geita aliyejulikana kwa jina la Rauson Lechapia anatuhumiwa kumshambulia kwa ngumi mwanafunzi wa kidato cha sita Jonathan Mkono hadi kupelekea kulazwa hospitali kutokana na maumivu makali. Kosa