Adui mkubwa wa walimu ni CWT.
NA RUSTON MSANGI. Adui ni kiumbe au mtu anayemtendea mwingine uovu, kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu. Uovu unaweza kuwa wa moja kwa moja au hata kwa njia ya kutotimiza majukumu vizuri. Chama cha walimu Tanzania CWT, ni miongoni mwa vyama vya wafanyakazi nchini, kinachoshughulika na walimu. Kwa mujibu wa katiba ya CWT, pamoja na madhumuni mengi ya chama hiki, jukumu kubwa na la pekee ni kusimamia hadhi, haki na maslahi ya walimu kitaaluma, kiuchumi, kijamii nk. Ni ukweli usiopingika kwamba ni vigumu kwa mwalimu mmojammoja kujitetea lakini kupitia umoja au taasisi ya CWT inakuwa rahisi zaidi. Kauli mbiu ya CWT ni HAKI na WAJIBU. Kwa miaka mingi kinachoangaliwa ni WAJIBU huku HAKI ikiwa imezikwa na kuachiwa kila mmoja kujitetea. CWT inaendeshwa kwa pesa za wanachama wake ambao ni walimu, kwa makato ya 2% ya mshahara kila mwisho wa mwezi. Hivyo kama ni rasilimali fedha ipo ya kutosha kufanya kazi kwa maslahi ya walimu. Nitakupa mfano kiduchu wa mapato ya CWT: