TATIZO SUGU LA MAJI MIKUMI LATAFUTIWA MUAROBAINI
MBUNGE WA MIKUMI ALIMAARUFU KWA JINA LA PROF JAY, AFANIKIWA KUPATA Sh. Milioni 208.6 ILI KUMALIZIA MRADI MKUBWA WA WORLD BANK KWENYE MJI MDOGO WA MIKUMI; Siku ya tar 5 february 2016 kwenye kikao cha Tisa cha Mkutano wa pili wa bunge la 11 Mbunge wa MIKUMI Mtumishi Joseph Leonard Haule Aliuliza swali la nyongeza kwenda Wizara ya MAJI NA UMWAGILIAJI Kuna tatizo sugu la maji kwenye jimbo la Mikumi , Je Serikali ina mpango gani wa kuondoa kero ya maji katika kata ya Mikumi, Ruaha, Uleling'ombe na maeneo ya Tindiga? ? MAJIBU ya Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji ni kama ifuatavyo; Mheshimiwa naibu spika na waheshimiwa wabunge, Mheshimiwa waziri katika majibu yake ametoa taarifa kwamba tunaingia katika program ya pili kupitia sera ya mwaka 2002 ya kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya watanzania wote watakuwa wanapata maji katika vijiji na asilimia 95 katika Miji. Mheshimiwa mbunge, Kwa upande wa jimbo lako la MIKUMI na kata zake, tutahakikisha kwamba tunazip