Posts

Walimu tujitafakari katika utoaji wa adhabu, hatma yetu iko mikononi mwetu

Image
NA RUSTON MSANGI. Kuna msemo unasema  kinga ni bora kuliko tiba, yaani ni bora uwe na tahadhari ya kukabiliana au kujihami na jambo lolote na si kusubiria hadi tatizo lijitokeze. Siku za hivi karibuni kumejitokeza matukio makubwa mawili nchini yanayohusisha walimu na wanafunzi. Tukio la kwanza ni la Agosti 27, 2018 ambapo mwalimu Respicius Patrick na mwenzake Herieth Gerald wa shule ya msingi Kibeta mkoani Kagera, wanatuhumiwa kwa kumuadhibu hadi kumsababishia kifo mwanafunzi wao Sperius Eradius wa darasa la tano. Chanzo cha tukio hili inasemekana ni mwanafunzi huyo kuhusishwa na wizi wa pochi ya mwalimu. Na hadi sasa walimu hawa wamesomewa mashtaka ya kuua kwa kukusudia katika kesi ya mauaji namba 18 ya mwaka 2018. Tukio lingine ni lile la mwalimu wa sekondari ya Kalangalala mkoani Geita aliyejulikana kwa jina la Rauson Lechapia anatuhumiwa kumshambulia kwa ngumi mwanafunzi wa kidato cha sita Jonathan Mkono hadi kupelekea kulazwa hospitali kutokana na maumivu makali. ...

Uchambuzi wa kifasihi katika wimbo wa Roma na Stamina uitwao Parapanda!

Image
NA RUSTON MSANGI. Fasihi ni sanaa itumiayo lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira/jamii iliyokusudiwa. Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum. Nyimbo huburudisha, kuelimisha, kusifia, kuliwaza nk. Hivi karibuni msanii Roma kwa mara nyingine, na kwasasa akiwa na mwenzake Stamina wamekonga nyoyo za mashabiki wa muziki na fasihi kwa ujumla kutokana na wimbo wao maarufu wa Parapanda. Wafuatiliaji wa mashairi ya Roma kwa muda mrefu, watakubaliana nami kwamba Roma amepiga hatua kubwa sana hasa katika matumizi ya fasihi. Katika wimbo huo wasanii Roma na Stamina wamekuja na aina tofauti kabisa. Wasanii hawa wamevaa uhusika wa watu wawili maarufu kwenye historia ya taifa letu, ambao kwa sasa hatuko nao hapa duniani. Yaani Baba wa taifa Mwal. Julius Kambarage Nyerere na Kingunge Ngombare Mwiru. Roma akiwa ni Nyerere na Stamina akivaa uhusika wa mzee Kingunge. Wasanii hawa wamefanya hivi kuvuta taswira juu ya mtazamo wa watu maarufu na ...

Wakuu wa shule wapata nafasi ya kukomoa walimu.

Image
NA RUSTON MSANGI. Ni wiki kadhaa sasa walimu wengi nchini wamekuwa katika msongo wa mawazo, hii ni kutokana na agizo la serikali linalotaka walimu wa sekondari wa stashahada na shahada wanaosemekana ni wa ziada kwa masomo ya sanaa wapelekwe shule za msingi. Mapema sana nilionesha kutokukubaliana na agizo hili kwa kuwa ni kimyume na mkataba, humuathiri mwalimu kisaikolojia, humshusha mwalimu cheo, hunyima wahusika ajira, nk. Katika utekelezaji wa agizo hili ambalo limepingwa na walimu wengi wenye akili, kumezuka matatizo makubwa zaidi. Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari nchini wamepata nafasi ya kuonyesha chuki za wazi kabisa kwa walimu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa namna moja au nyingine wakuu wa shule wamehusika moja kwa moja katika zoezi la kuhamisha walimu kutoka sekondari kwenda shule za msingi. Na ushiriki wa wakuu wa shule haujawa wa heri wala haki, bali imekuwa ni nafasi kwao kuadhibu, kukomoa na kuondoa watu ambao wanahisi ni kero kwao. Nayasema hay...

Adui mkubwa wa walimu ni CWT.

Image
NA RUSTON MSANGI. Adui ni kiumbe au mtu anayemtendea mwingine uovu, kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu. Uovu unaweza kuwa wa moja kwa moja au hata kwa njia ya kutotimiza majukumu vizuri. Chama cha walimu Tanzania CWT,  ni miongoni mwa vyama vya wafanyakazi nchini, kinachoshughulika na walimu. Kwa mujibu wa katiba ya CWT, pamoja na madhumuni mengi ya chama hiki, jukumu kubwa na la pekee ni kusimamia hadhi, haki na maslahi ya walimu kitaaluma, kiuchumi, kijamii nk. Ni ukweli usiopingika kwamba ni vigumu kwa mwalimu mmojammoja kujitetea lakini kupitia umoja au taasisi ya CWT inakuwa rahisi zaidi. Kauli mbiu ya CWT ni HAKI na WAJIBU. Kwa miaka mingi kinachoangaliwa ni WAJIBU huku HAKI ikiwa imezikwa na kuachiwa kila mmoja kujitetea. CWT inaendeshwa kwa pesa za wanachama wake ambao ni walimu, kwa makato ya 2% ya mshahara kila mwisho wa mwezi. Hivyo kama ni rasilimali fedha ipo ya kutosha kufanya kazi kwa maslahi ya walimu. Nitakupa mfano kiduchu wa mapato ya CW...

Mohamed Hamisi ni mlemavu mwenye malengo makubwa na yenye tija

Image
Pichan:Mlemavu anayependa kujishughulisha Pichan:Mh Ally Bananga Diwani wa kata ya Sombetini kupitia Chadema akiwa na Mohamed Hamisi ambaye ni mlemavu mwenye nia ya kujishughulisha badala ya kuishi kama omba omba wakijadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo Mohamed Hamisi ni mkazi wa Sombetini. Ana umri wa miaka 24. Ni mtoto wa marehemu Hamisi Faustine. Ni mlemavu wa miguu na mkono mmoja pia una shida. Hapendi kuomba, anapenda kujishughulisha. Kwa sasa anafanya vikazi vidogo vidogo vya kuweka tinted kwenye magari lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa.   Anatamani  kuwa na biashara nyingine ndogo ili aweze kuongeza kipato kuwasaidia wadogo zake watano ambapo mdogo kabisa ana miaka minne.    Anaomba msaada afungue ofisi yake ili achanganye kazi zake ya kuweka tinted (maana sasa anafanya kwa mtu) na pia ofisi hiyo ataweza kuongeza biashara nyingine ya kuuza na kuburn VCD, kuuza mitumba vocha na kadhalika. Pia baiskeli yake ni nzito, ni ya mbao na chuma has...