Posts

UKAWA INATAKA KUSHINDA AU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU 2015?

Image
UKAWA inataka kushinda Uchaguzi au inataka Kushiriki Uchaguzi? Yericko Nyerere  Kushindwa kwa upinzani nchni kwa kiwango kikubwa katika chaguzi hizi kunatokana na muundo wa vyombo vya maamuzi ya uchaguzi wa nchi yetu, mathalani, Katiba, Tume. Kwasasa Katiba inasema kuwa matokeo ya urais hayatahojiwa na mtu yeyote ama chombo chochote wala mahali popote, hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa Tume anayechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM na anayelipwa na Mwenyekiti wa ccm akitangaza jina fulani hata kwa bahati mbaya tu baai haruhusiwi kurekebisha. Mwaka 2010 baada ya kushindwa uchaguzi mkuu, Upinzani chini ya Chadema uliituhumu sana tume Uchaguzi kwakuchakachua matokeo ambayo ilipoka ushindi wa 64% wa Dr Slaa malalamiko yao ndiyo yalipelekea kuwepo mchakato wa kuandika katiba mpya. Mchakato huo umeishia kwa zengwe la CCM kuvuruga maoni ya umma na kuweka maoni yao ambayo ni kinyume kabisa na matakwa ya umma, Maridhiano ya upinzani na msanii wa ccm baada ya dalili za uwepo finyu wa ...

Mh.KAFULILA AWALIPUA MAWAZIRI UFISADI MABEHEWA, ALITAKA BUNGE KUWAJIBISHA VIGOGO UFISADI WA MABEHEWA

Image
Na Shindo Kilawa Pichani ni Mh KAFULILA 

BENSON KIGAILA AONESHA UWEZO WA KIPEKEE KATIKA KUPAMBANUA MAMBO

Na Mhere Mwita Majira ya saa 2:30 Ndugu Benson Kigaila ambaye ni mkurugenzi wa organization ya CHADEMA ngazi ya Taifa na ni mtia nia ubunge jimbo la Dodoma mjini alifanikiwa kufanya mdahalo na wanachama ,baadhi ya viongozi na watia nia wa  Ubunge na Udiwani toka sehemu mbalimbali za nchi.Kijana haya alijidhihirisha kuwa anauwezo wa kipekee na ana kaliba ya kiuongozi kwa kujib maswali kwa ufasaha zaidi ya matarajio ya wengi. Uwezo wake ulitambulisha kuwa CHADEMA ina hazina kubwa ya viongozi tens waliomakini nitaweka baadhi ya maswali na majibu aliyoulizwa na wajumbe hao hapa chini:- swali 1:Kwanini umeamua kugombea ubunge? Majibu:Nimeamua kugombea ubunge kwa lengo la kusaidia kujenga jamii ya watu walio sawa mbele ya sharia,jamii guru na inayongozwa kwa haki na kuwatatulia kero zinazowakabili sasa ambazo waliopita hawajazitatua hadi leo kwa mfano Tatizo la Ardhi ya watu wa Dodoma dhidi ya CDA,ni tatizo kubwa linalohitaji mtu anayelijua na ana dhamira ya dhati kulitatua aliwe...

RAIS WA MAREKANI BARAKI OBAMA AKERWA NA MAUAJI YA WAMAREKANI WEUSI, AMESIKITISHWA SANA NA KITENDO HICHO CHA KIKATILI NA KIBAGUZI

Image
Rais wa Marekani (USA) Barak Obama amesema mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa Wamarekani Weusi katika eneo la Charleston, jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali mengi sana Aidha Mh Barak Obama amesema chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa demokrasia ya Marekani amelaani vikali kitendo hicho na vitendo vingine vinavyoweza kuhatarisha umoja wao, ameyasema hayo mda mfupi baada ya kijana wa kizungu aliyehusika kufanya mauaji hayo ya watu tisa kukamatwa. Pia ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.

KAFULILA: JK KAVUNJA MISINGI YA UCHUMI ALOWEKA MKAPA.

Image
Na Mh Kafulila Huu ndio mchango wangu bungeni jioni leo.Mkapa aliweka misingi ya uchumi mkuu( macro economics) kilichopaswa kufanywa na JK ni kuhakikisha mafanikio hayo yanajitokeza kwenye uchumi wa kawaida ili kila mtanzania aone fahari ya kukua kwa uchumi wake lakn bahati mbaya amebomoa kabisa na sasa inabidi UKAWA tuanze upya baada ya uchaguzi Oct. 1. Mkapa amepokea nchi mwaka 1995  ukuaji wa uchumi ukiwa 4.2 akakuza mpaka 6.7 mwaka 2004. Leo JK kashusha uchumi mpaka 6.4 mwaka 2014. 2. Amepokea nchi riba ya mabenki ikiwa 30-26% mwaka 1995 lakn mwaka 2005 riba za mabenki ilishuka hadi 14% lakn leo JK riba zimepanda mpaka 18%. Hii inathiri sana ukuaji wa sekta binafsi na biashara nchini. 3.Mwaka 1995 mfumko wa bei ulikuwa 21% lakn mwaka 2005 mfumko ulishuka mpaka 4%. Leo JK mfumko wa bei ni 5.3% .  4. Mkapa kapewa nchi mwaka 1995 akiba ya fedha za kigeni zikiwa za miezi 2 lakn mwaka 2005 akiba ilikuwa ya miezi 8 lakn leo mwaka 2015 akiba za pesa za kige...