Posts

MASOKO YA MTWARA MIKINDANI YAKABILIWA NA TATIZO LA VYOO

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la kijiji cha mkunjanguo katika kata ya Naliendele mkoani Mtwara wamelalamikia ukosefu wa huduma muhimu ikiwemo choo katika soko hilo. Wakizungumza  sokoni hapo na mwandishi wa habari hii baadhi ya wafanyabiashara hao wamesema kuwa  changamoto hiyo imekuwepo sokoni hapo kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwapa usumbufu mkubwa na kuwaweka katika hatari ya magonjwa ya milipuko katika eneo hilo. Uongozi wa eneo hilo akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa eneo hilo halikidhi vigezo vya kuwa soko na kuwa na kuwa awali mzabuni ambaye alipewa dhamana ya soko hilo alishindwa kujenga vyoo sokoni hapo.  Hata hivyo ameongeza kuwa jitihada zinaendelea kuhakikisha soko hilo linapata vyoo na kuwa wataanzisha utaratibu mpya wa kutoza ili kuwezesha kujenga vyoo hivyo. Aidha masoko mengi katika manispaa ya Mtwara mikindani  yanakabiliwa na uhaba wa vyoo bora jambo ambalo linatis...

CHAMA CHA USHIRIKA MKOANI MTWARA CHAWATAKA WAFANYA BIASHARA WA MAZAO KUFUATA MISINGI NA TARATIBU ZA KIBIASHARA

Chama cha ushirika wa wakulima mkoani Mtwara kimewataka wanunuzi wa mazao mbalimbali kuacha kutumia mizani kwa kuwa ni kosa kisheria na ni unyonyaji kwa wakulima. Wito huo umetolewa na Kamimu Mkurugenzi wa chama hicho mkoani hapa Bw. Laurence Njozi ambapo amesema kuwa chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobanika kufanya manunuzi kwa njia hiyo isiyo halali. Amesema kuwa ili kuepukana na tatizo hilo pia ni vema kwa wakulima kuwa na subira ya kuuza mazao yao ghalani na kuachana na utaratibu wa kuuza reja reja kwa kuwa unawaumiza. Ameongeza kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya wakulima kukosa uvumilivu kwa kucheleweshewa malipo yao pamoja na wanunuzi hao wadogo ambao hununua kinyume cha sheria. Aidha serikali imepiga marufuku uuzaji wa mazao kwa kutumia mizani kwa wanunuzi wa reja reja na kujaza rumbesa kwa kuwa inawanyonya wakulima.

MAKAMU MWENYEKITI BAVICHA BARA MH PATRICK OLE SOSOPI AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA

Image
Tayari Jeshi la  Polisi limemkamata Makamu M/kiti wa BAVICHA muda huu hapa Iringa Mjini baada tu ya kumaliza Mahafali ya CHASO. Kosa ni la uchochezi wa Kisiasa ambalo alilitenda akiwa DSM katika Mahafali ya CHASO ya tarehe 18/06/2016. Hivyo atasafirishwa kutoka Iringa kwenda DSM kwaajili ya mahojiano na baadae Mahakamani. Imetolewa June 26 Edward Simbeye Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa

DHANA YA UONGOZI NA UTAWALA WA SHERIA TANZANIA

Image
Na Emmanuel Chengula, Kiongozi ni mtu ambaye amechaguliwa na watu katika jamii ili awaonyeshe njia ya kutatua matatizo, namna ya kuhitajiana katika kuishi na namna ya kuangalia changamoto zinazoikumba jamii na kuzitatua. Aidha kiongozi hutengenezwa ama pengine mtu huzaliwa akiwa kiongozi. Utawala wa sheria ni ile hali ya uongozi kuhakikisha kwamba kila jambo linaloamuliwa kufanywa na jamii ama na uongozi uliopo unafuata misingi ya haki na utawala bora kwa mujbu wa sheria za nchi zilizopo. Inafahamika kwamba mara zote kiongozi wa mwisho katika nchi nyingi huwa ni rais/mfalme n.k na kauli zao mara nyingi zitolewapo huchukuliwa kama sheria(presidential decree/orders) ndani ya jamii husika. Sheria za jamhuri ya Muungano wa Tanzania zipo open sana mfano ukisoma ibara ya 13(6) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema every person is presumed innocent unless proved contrary ( yaani kila mtuhumiwa katika jamii hudhaniea hana kosa mpaka pale itakapothibitka kwamba kafanya...

MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MH BONIFACE JACOB AFUNGUKA JIONI YA LEO

Image
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA MSTAHIKI MEYA BONIFACE JACOB Asalaam aleikum wananchi wa wilaya ya kinondoni na viunga vyake, niendelee kuwaombea ndugu zetu waislamu funga yao iwe na heri na baraka tele ikiwa leo ni chungu cha 19. Leo tarehe 25 june 2016, nimepigiwa simu nyingi sana na kupokea taarifa kwa njia mbalimbali, nikiulizwa nilipo? kwanini sipo kwenye tukio la Biafra la uzinduzi wa shughuli ya jeshi la polisi? na wengine wakiniuliza neno baada ya kuuliziwa hadharani na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. MHESHIMIWA RAIS John pombe Magufuli; Mstahiki meya manispaa ya kinondoni leo siku ya jumamosi kijana wako na mtumishi wa wananchi wa manipsaa ya kinondoni nilikuwa naunga mkono shughuli za usafi. Nimeshinda na wananchi wa ubungo kisiwani kutwa tukifukua mitaro ya maji machafu kuhakikisha usalama wa afya za ubungo kisiwani zipo salama na zaidi kuweka miundo mbinu yetu sawa. Nami nilitamani sana kukuona japo kwa karibu sana au kuongea na wewe mambo kadhaa k...