Posts

UGONJWA WA KISUKARI UNAVYOPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

Image
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) huambatana na ongezeko la sukari(glucose) katika damu kwa kiwango kinachozidi kawaida. Homoni aina ya insulin ambayo hutolewa na kongosho ama hushindwa kufanya kazi yake vema kwa sababu ya kasoro za seli au hutolewa kwa kiasi kisicho kidhi uhitaji wa kuratibu sukari katika damu. Kwa hivyo sukari hubaki katika damu kwa wingi na kuleta madhara kadhaa.Wagonjwa wa kisukari pia huweza kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) katika damu. Na zaidi huweza kuwa na tatizo la mgandamizo wa damu (hypertension) au presha. Asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume. Mambo haya matatu, Sukari, lehemu (Cholesterol) na Mgandamizo wa damu, Huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.(Erection dysfunction). 1. Sukari. Sukari nyingi katika damu huweza kupelekea kuharibiwa kwa kuta za mishipa ya damu. Kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitish...

MEYA WA KINONDONI AGAWA BURE MAENEO YA BIASHARA ASUBUHI YA LEO

Image
Meya akiongea na wafanyabiashara leo la asubuhi Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo Ijumaa 29/04/2016 amefanya ziara katika eneo la ubungo na kuongea na wafanyabiashara ikiwemo kuwaonyesha eneo la kufanya biashara zao. Amewataka wafanyabiashara hao kesho wasiwepo maeneo hayo na kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza), kwani wasipofanya hivyo Kamati ya usalama na ulinzi  na usalama Manispaa ya Kinondoni imeshakaa na imepanga kuwaondoa. Meya ameona isingekuwa busara kuwaondoa bila kujua watakwenda wapi, Meya amewakabidhi wafanyabiashara hao kadi ambazo watazionyesha ili  wasisumbuliwe,pia amewataka wasilipe pesa yeyote endapo watatakiwa walipie maeneo ya biashara waliyopewa. Pia amesema kuhusu ushuru hawatalipa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo watalipia, amewahakikishia wafanyabiashara hao hakuna atakayekosa eneo la kufanya biashara. Afisa biashara wa Manispaa ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara kutokaidi agiz...

WAAJIRI KATIKA TAASISI MBALIMBALI WILAYANI MTWARA WAMETAKIWA KULIPA WAFANYA KAZI WAO UJIRA KULINGANA NA KAZI WANAZO FANYA

Image
Wamiliki na waaajiri katika taasisi mbalimbali wilayani mtwara wametakiwa kuwajali na kuthamini michango ya wafanya kazi wao kwa kuangalia kazi wanazofanya na zilingane na mishahara wanayowapatia kwa mwezi. Akitoa wito huo katika mahafali ya wahitimu wa huduma za hotelini yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Old Boma mikindani mkuu wa wilaya mtwara Bi Fatuma Alli amesema kuwa wafanya kazi wengi katika hoteli zilizopo mjini mtwara hawalipwi ujira mkubwa kulingana na kazi wanazofanya na kupelekea kuwepo kwa vitendo visivyo vya kimaadili katika maeneo yao ya kazi. Bi Fatuma Alli amewataka wahitimu hao kuheshimu mikataba wanayopewa na waajiri wao kwa kuwa na nidhamu ,heshima,Busara na kuendana na maadili ya kitanzania wakiwa katika huduma zao kwa wateja na wafanya kazi wengine. Mkuu huyo wa wilaya pia amewataka wahitimu hao kujiendeleza kielimu ili kuendana soka la ajira la hivi sasa nchini na Dunia kwa ujumla,N a kuwashauri kama vijana kuwa tayari kukabiliana na mabadil...

MAISHA NA UGONJWA WA KISUKARI

Image
Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus) ni ugonjwa sugu unaotokea wakati fisiolojia ya mwili inaposhindwa kuratibu kiwango cha sukari katika damu. HIvyo sukari hupanda kwa kiasi kinachozidi kawaida na kusababisha matokeo hasi mbalimbali mwilini. Baadhi ya matokeo hasi yanayoletwa na kisukari ni Kupatwa na mgandamizo wa damu (presha), Upofu unaosababishwa na kuharibika kwa Retina ya jicho (retinopathy), magonjwa ya figo (nephropathy), magonjwa ya neva za fahamu (neuropathy), Kuharibika kwa mirija ya damu (diabetic angiopathy) nk. Magonjwa ya neva za fahamu na mirija ya damu huweza kusababisha vidonda sugu visivyopona na kupelekea ulazima wa kukatwa mguu au mkono kutegemea na eneo kilipo kidonda. Kwa hiyo moja kati ya changamoto kubwa kwa mgonjwa wa kisukari ni kuepuka majeraha. Njia mbali mbali zaweza kusaidia kuepuka matokeo hasi ya ugonjwa wa kisukari. 1. Kuacha kabisa kuvuta sigara. 2. Kufanya mazoezi mepesi (aerobic exercise) ili kuchangamsha mzunguko wa damu. 3.Kupunguza ku...

LEICESTER CITY KUITIA HASARA KAMPUNI YA KAMALI

Image
Timu LEICESTER CITY wakishangilia goli katika moja ya mechi zao. Kushoto chini ni Washambuliaji, Vardya na Mahrez. Kulia ni Leigh Hebert, mashabiki anayesubiri kushinda kitita cha Pauni 25,000 endapo timu yake ya LEICESTER CITY itabeba ubingwa wa ligi kuu msimu huu.                                                           Mazoezi ya LEICESTER CITY. Endapo LEICESTER CITY itashinda kombe la ligi kuu Uingereza msimu huu, basi fundi seremala kutoka kitongoji cha Guildford huko Uingereza atashinda kiasi cha pound 25,000, zaidi ya Tsh milioni 75 baada ya kuweka 'bid' ya paund 5 (Tsh. Elfu 15) kwenye mchezo wa kamali; Fundi Leigh Hebert, amekataa ofa ya paund 3200 (Tsh milioni 9.6) aliyopewa na kampuni hiyo ya kamali ili aondoe utabiri wake na kusema anataka kushinda paund zote 25000 au hata akipoteza paund 5 aliyoweka haina noma. ...