Posts

SAMSON MWIGAMBA AJIUZULU NAFASI YAKE YA UKATIBU MKUU ACT - WAZALENDO

Image
Pichani ni mh Mwigamba katibu mkuu wa ACT wazalendo aliyejiuzulu  nafasi yake kwa sababu anakwenda masomoni nchini Kenya  Katibu mkuu wa chama cha ACT wazalendo Samson Mwigamba ameamua kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu mkuu wa chama. Mwigamba anasema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa sababu anakwenda masomoni inchini Kenya. Kamati ya uongozi wa chama chake wameridhia na kupokea maombi ya katibu huyo, zaidi wamempongeza kwa juhudi zake na uwezo wake katika harakati za kukikuza chama hicho cha upinzani nchini Tanzania, Aidha Mwigamba anasema yeye atabaki kuwa mwanachama hai wa chama cha ACT wazalendo na atashirikiana na wanachama wenzake na viongozi kwa ujumla katika kuendeleza harakati za kukitangaza na kukieneza chama chao nchini na amewashukuru viongozi wenzake, wanachama wenzake na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano wao. Kwa mjibu wa kamati ya uongozi machamato wa kupata katibu mwingine utatangazwa wakati wowote ili mtu mwingine aendeleze harakati za kukijenga...

ELIMU BURE NA CHANGAMOTO HASI.. SERIKALI ITAZAME UPYA MPANGO HUU!!

TATIZO ninaloliona nchini kwetu baada ya uchaguzi kumalizika hadi sasa miezi 7 baada ya serikali ya Rais Magufuli kuapishwa ni kuwa kuna watu wengi tunaimani na MAGUFULI.. Labda kwa kuwa anaonyesha utofauti mkubwa wa kiutendaji na watangulizi wake wengine waliopita, ni HAKI YAKE SISI kumuunga mkono, maana ni Rais wa Nchi yetu ya Tanzania. Lakini tatizo linakuja kwa wachache wenye imani kubwa kupita kiasi, kufikia hatua ya chochote anachokosolewa (Magufuli) yeye na serikali yake, wao wanafikiri ni kuwa watu wanamtafutia ubaya au hawapendi afanikiwe.... laah! Hasha.. SIYO KWELI. Rais Magufuli akiharibikiwa na sisi pia tumeharibikiwa maana ndiye kiongozi mkuu wa nchi yetu.., ndiye mwenye kubeba dira na matakwa ya watanzania.. Mfano mdogo sana ambao mimi binafsi mwanzoni mwa mwaka huu niliupigia kelele sana; hii 'issue' ya Elimu bure.. January mwaka huu kama ilivyotangazwa na ofisi ya Rais baadaye wizara ya elimu, kwamba wanafunzi wapate elinu yao bure.. kuanzia ...

Thomas Isidore Nöel Sankara Taa ya Afrika iliyozimika ghafla!

Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas Sankara  na Blasius Compaore, waliipindua serikali ya Rais wa wakati huo katika nchi iliyokuwa ikijulikana kama Upper volta, rais huyu aliitwa Baptiste Ouedraogo... Vijana hawa wakiwa katika fikra za Karl Max, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga Upper volta.., walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, manake nchi ya watu, country of honorable citizen.. Uchapa kazi wa vijana hawa (Sankara na Compaore), Thomas sankara akiwa ndiye rais unaweza kufananishwa na ule wa Fider Castrol na Che Guavera, kabla haujachuja kule Cuba.. Haiyumkini Sankara alikuwa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake (Compaore) wakiwa kama pete na kidole.. Urafiki wa makapteni hawa wa jeshi la Burkinabe, ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama walipomwambia Sankara kuwa Compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua, yeye aliwaji...

HOFU NI SEHEMU YA UTASHI WA BINADAMU.. UOGA NI DHAMBI UKITAWALA.

Kwa kawaida mtu mwenye wasiwasi akionyesha wasiwasi wake ni vizuri kumpatia majibu ya kumwondoa katika wasiwasi huo ili kuepusha migongano inayo weza kuleta migogoro. Nakumbushwa kuwa Mwanafalsafa wa kutoka Derbyshire, England Thomas Hobbes, alizaliwa 1558 na kufariki 1679 akiwa na umri wa miaka 91 alibainisha, kuwa migogoro mingi miongoni mwetu hutokana na ushindani wa kugombania kisichotosha. Kwa vile sote tuna mahitaji yenye kufanana, basi Mwanafalsa huyu alisema kuwa migogoro hii itaendelea. Mwanafalsafa huyu aliamini kuwa kutokana na hatari hii, basi jukumu muhimu na kubwa kwa Serikali yeyote ile iwe ni kulinda amani ya nchi. Kwamba kwa kutofanya hivyo, jamii itarudi katika hali ya kutokuwa na taratibu. Nitaendelea kuamini kuwa siku zote, pasipo haki na usawa hakuna amani,... Ingawa katika jamii yeyote ile, uwepo wa amani na utulivu ni msingi mzuri katika kutafuta haki na usawa, kwa njia ya majadiliano. Nilipata kusoma kisa cha mtego wa panya uliosababisha madhara...

PATA MAGAZETI YA LEO JUMATANO YA TR 20/04/2016

Image