LEO NI SIKU YA KIHISTORIA KUANZA HATUA NYINGINE YA KUMALIZA DHULUMA YA KISIASA VISIWANI ZANZIBAR
Naangalia Star Tv, Leo ni siku ya kihistoria kuanza hatua nyingine ya kumaliza dhuluma ya kisiasa visiwani Zanzibar Na Ben Saa Nane Maalim Seif Shariff Hamad anatangazwa leo kuwa Mgombea Urais wa Chama cha CUF mshirika Mwenza wa UKAWA katika kinyang'anyiro cha Urais wa Zanzibar Issa Bin Nasser katika kitabu chake "Zanzibar:Kinyang'anyiro na Utumwa" aliandika maneno haya "Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye yote na ndiye atakayemua na kuhukumu kwa haki" .Ni baada ya kuichambua dhuluma ambayo Zanzibar na wazanzibar wamekua wakifanyiwa Maalim Seif Shariff na Chama chake cha CUF wamekua mstari wa mbele kupambana na Dhuluma hii Binafsi katika ukuaji wangu kisiasa nimekua nikimhusudu sana Maalim Seif Sharif Hammad kwa misimamo mikali na uzalendo wa kile anachopigania kuhusu Zanzibar na Watu wake Ni mwanamapinduzi asiyeyumbishwa Wanasiasa wa aina hii ni nadra sana na kadiri nilivyozidi kuzama ndani na kukomaa kisiasa nilikuja kugundua ni kwanini mtu kama M...