MALEZI YA MTOTO, DEMOKRASIA NA HATIMA YA MAENDELEO YA NCHI YETU.
Na Dr. Elias Mwakapimba Katika malezi ya mtoto kuna vitu vingi ambavyo vinaathiri afya kwa ukuaji mzuri. Vitu hivi ni elemu/uelewa wa mzazi, uwezo wao wa kiuchumi/kipato na mazingira wanamoishi. Haya mambo ni nguzo muhimu katika kuimarisha afya thabiti kwa ukuaji na mafanikio ya mtoto baadaye. Wazazi wa mtoto wanaweza kuwa na elimu/uelewa wa kulea mtoto lakini hawana uwezo wa kumudu mahitaji kwa afya njema ya mtoto. Wanaweza wakawa na kipato kizuri lakini wasiwe na elimu/uelewa wa namna ya kuanda lishe nzuri ya mtoto. Au wanaweza wakawa navyo vyote lakini mazingira yasiwe rafiki katika kuandaa lishe ambayo ni muhimu kwa afya ya mtoto (mfano vita/ukimbizi) au wakaweza kuandaa lishe lakini mazingira tena yasiwe rafiki kuruhusu mtoto kufaidi virutubisho vya lishe na asiweze kukua katika afya (mfano magonjwa). Katika makundi mawili ya awali: ukosefu wa elimu au kipato, au ukosefu wa vyote au uwepo wa vyote lakini mazingira yasiwe rafiki hupelekea mtoto kuwa na utapia mlo (mtoto