Walimu wa mwaka 1993 ni mfano wa kuigwa
NA RUSTON MSANGI.
Katika historia ya harakati za walimu nchini, inaonesha kwamba mwaka 1993 kulitokea mgomo wa walimu.
Kipindi hiki ulikuwa utawala wa awamu ya pili chini ya Rais Ally Hassan Mwinyi. Mgomo huu ulitokana na madai lukuki ya walimu dhidi ya Serikali, kama ilivyo sasa.
Kinara wa mgomo huo alikuwa Mwalimu Peter Lebabu Mashanga, huyu alikuwa ni mwenyekiti wa OTTU (Organization of Tanzania Trade Unions) tawi la Azania sekondari.
Mwalimu Peter Lebabu Mashanga akiungwa mkono na walimu wa Dar es Salaam mnamo October 1993, walimuandikia Rais Ally Hassan Mwinyi barua, wakieleza madai 14 ya walimu na kumpa muda maalum wa kutekeleza madai hayo. Vinginevyo wangegoma nchi nzima ikifika 1/11/1993 hadi madai yatakapotekelezwa.
Madai haya ya walimu ya mwaka 1993 yalijulikana kama ''Pan African Tanzania Teachers Demands''. Na madai yenyewe baadhi ni kama ifuatavyo:-
1. Comprehensive medical care.
2. Emergency medical fund amounting to 60,000 p.m
3. Lunch allowance amounting to 60,000 p.m
4. Transport allowance amounting to 60,000 p.m
5. Housing allowance amounting to 60,000 p.m
6. Hardship allowance amounting to 30,000 p.m
7. Fare allowance in cash in place/instead of warrants
8. Employing authority to meet the cost of a member of service and his /her dependants who died in Tanzania such express shall include but not limited to the cost of: coffin, grave, shroud, wreath.
9. All teachers must have undergone Teacher training course and should have a teaching lecence.
10. Evaluation compensation. The Tanzania shilling has been devaluing relentlessly as per the shown mathematical reality as from 1961,
$ 1 = Tsh 20/= in 1961
$ 1= Tsh 750/= in 1993.
Hayo ni baadhi ya madai ya walimu ya mwaka 1993 yaliyopokelewa na rais Ally Hassan Mwinyi.
Pamoja na rais kupokea madai haya ya walimu, hakuna hata kimoja kilichotekelezwa.
Walimu kote nchini waliwaunga mkono walimu wa mkoa wa Dar es Salaam katika mgomo huo.
Baadhi ya walimu wanaokadiriwa kufikia 200 walifukuzwa kazi kwasababu ya kugoma kwa ajili ya kudai haki zao ambazo ziko kisheria. (Baadae walirudishwa kazini bila masharti yoyote)
Pamoja na madai hayo kutotekelezwa, Rais alitoa majibu mepesi yenye misingi ya hoja mbili zifuatazo,-
Mosi, Rais alisema madai ya walimu ni mamilioni ya pesa ambayo Serikali haitaweza kuyalipa.
Mbili, Rais alisema hawezi kushugulikia madai ya walimu bila uwepo chama rasmi cha walimu.
Majibu ya rais hayo ya mwaka 1993, yaliwafanya walimu kurudi nyuma na kusitisha mgomo ili kupata nafasi ya kusajili Chama cha Walimu Tanzania (CWT)rasmi.
Ikumbukwe wakati harakati hizi za mgomo walimu zikifanyika, kulikuwa hakuna chama rasmi cha walimu kama ilivyo sasa.
Vilevile ikumbukwe kulikuwa hakuna idadi ya walimu waliopo sasa na wenye taaluma kama zilizopo sasa.
Leo tuna chama cha walimu Tanzania CWT, tuna michango ya 2% kila mwezi kwa kila mwlaimu kwa ajili ya kazi za chama, na kazi kubwa ni kutetea haki za wanachama wake, ambao ni Walimu.
Kada ya walimu ni kadi yenye watumishi wengi nchini kuliko kada yoyote ile. Hivyohivyo ndo kada pekee yenye madai mengi kuliko kada yoyote ile.
Kwa namna madeni yanavyozidi, makato yanavyozidi, hali ngumu inavyozidi, manyanyaso yanvyozidi. Nina wasiwasi kuna siku serikali itasema haiwezi kulipa madeni ya walimu kwa kuwa ni makubwa sana.
Madai mengi ya walimu yako kisheria, na mazingira yanalazimisha walimu kudai vitu vingine vingi.
Huu ni wakati sasa wa CWT kuiga mfano wa walimu wa mwaka 1993. Hakika walimu hawa ni mfano wa kuigwa na kizazi cha sasa na vizazi vingi vijavyo.
Mwalimu Peter Lababu Mashanga, popote ulipo kwa sasa utakumbukwa daima kwa misimamo na ujasiri wako katika kupigania haki zako na za walimu wenzako. U are a true soldier.
Mwandishi ni mchambuzi wa masuala ya Elimu.
Namba yake ya simu:0684 731516
Barua pepe:rustonmsangi@yahoo.com
Comments
Post a Comment