WOGA UNAVYOWATESA WALIMU!
NA RUSTON MSANGI. Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu toleo la pili, 2004, Woga ni hali ya kuwa na hofu ya kufikwa na jambo la kutisha au la taabu. Hali ya kutoweza kustahimili vitisho, hofu. Waajiriwa wote ulimwenguni wanapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu. Wakiwa wanatimiza wajibu wao na kupata haki zao bila mateso na manyanyaso yoyote ndani na nje ya eneo la kazi. Nchini Tanzania hali iko tofauti sana kwa wafanyakazi wengi, hususani WALIMU, ambayo ni kada pekee yenye watumishi wengi nchini. Kwa muda mrefu sana walimu wamekuwa ni kundi pekee ambalo kila kiongozi wa nchi hii anaona ni sehemu ya kuchukulia umaarufu. Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, viongozi wa kata, viongozi wa CCM nk, Kwa muda mrefu kwa nyakati tofauti wamekuwa wakimtumia Mwalimu kama sehemu ya kujaribia utendaji wao. Manyanyaso, udhalilishaji na ukandamizwaji kwa Walimu sio kwamba walimu wanaupenda na kukubali, bali ni WOGA tu unawasumbua walimu wengi. Matukio mengi ya kud