Ufaulu hauji kwa kufanya kazi kama watumwa!
NA RUSTON MSANGI. Shughuli yoyote ile ya kimaendeleo inapofanyika, hutegemewa kuwa na matokeo chanya. Hadi kufikia matokeo yanayohitajika, njia za aina tofauti tofauti hutumiwa kufikia mafanikio. Ubora au ubaya wa njia itakayotumika inategemeana kwa kiasi kikubwa na uongozi wa wa shughuli au eneo husika. Vivyo hivyo katika mfumo mzima wa elimu nchini Tanzania, shuleni tunapopeleka vijana/wanafunzi wetu kupata maarifa tunatarajia wapate matokeo mazuri na kufaulu mitihani yao. Ili ufaulu unaotarajiwa uweze kupatikana kwa wanafunzi wetu, wasimamizi wa elimu na viongozi wa Shule wanategemewa kuwa na mbinu, maarifa, weledi na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa walimu ambao ndiyo watekelezaji wakuu wa sera na mipango ya elimu. Hivyo kukiwa na mipango mizuri kwa ushirikiano, hata matokeo yatakuwa mazuri. Kutokana na umuhimu wa elimu nchini, nalazimika kuzungumzia ufaulu, namna ya kufanikisha na vikwazo vilivyopo kwa wasimamizi hasa mashuleni kama ambavyo kila kukicha yanajitokez