KUCHELEWA KWA AJIRA KUNAVYOUMIZA WALIMU
NA RUSTON MSANGI. Kada ya ualimu ndiyo yenye watumishi wengi nchini kuliko kada yoyote ile. Licha ya kada hii kuwa na watumishi wengi,takwimu zinaonesha bado kuna upungufu wa walimu nchini hasa walimu wa sayansi . Waziri mwenye dhamana ya elimu,Profesa Joyce Ndalichako akijibu swali katika kikao cha bunge kilichopita, alibainisha upungufu wa walimu wa Sayansi 22,460. Miaka kadhaa iliyopita,watu wengi wamepata hamasa ya kusomea fani ya ualimu ili waajiriwe na serikali.Hakika walimu wamekuwa wakiajiriwa moja kwa moja katika shule katika shule za msingi na sekondari na vyuo . Walimu wamekuwa wakiajiriwa kwa vipindi tofauti mara wa wanapohitimu. Kwa mfano, walimu waliohitimu mwaka 2012 walipangiwa vituo vya kazi mwezi Februari 2013. Waliohitimu mwaka 2013 walipangiwa mwezi Machi 2014 na waliomaliza mwaka 2014 walipangiwa mwezi wa tano 2015. Lakini mamia ya walimu waliohitimu mwaka 2015 ,hawajaajiriwa,wanaendelea kusota mitaani.Kuchelewa sana kwa ajira za ualimu kumekithiri kat